Katibu mkuu CHADEMA, Mnyika umetegwa ukitegeka nafasi yako wanachukua wenye chama chao

Katibu mkuu CHADEMA, Mnyika umetegwa ukitegeka nafasi yako wanachukua wenye chama chao

OTTER

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
476
Reaction score
330
Mh. Mnyika Katibu Mkuu CHADEMA, kwa sasa wajumbe wa Kamati kuu wanakuangalia kwa pande mbili, pande ya kwanza kukikosesha chama kupata ruzuku kwa kutopeleka majina ya wabunge viti maalum, upande wa pili kuwasababishia wanachama kukosa ajira ya uteuzi wa kuwakilisha hoja za chama chenu bungeni.

Ukikosea mahesabu hayo, hiyo nafasi watapewa wenye chama muda si mrefu. Zakuambiwa changanya na zakwako.

Maendeleo hayana Chama
 
Boss wenu alisema hataki kuchanganyiwa betri na magunzi wakati wa kampeni zake, Baada ya kuona mambo yanawaendea ndivyo sivyo mnaanza tena kutafuta magunzi ili muchanganye. Kwanini msitafute magunzi toka wasanii wa bongo movie, Polisi, TISS na wengine wote waliowasaidia kupora haki ya Watanzania?
 
Kijana hodari na mchapakazi,na hakika atarudi nyumbani na atapewa teuzi kama shukrani kwake,wala asiwaze kipigwa chini na wafipa.
 
Unajua wajibu na majukumu ya katibu mkuu?

Mojawapo kubwa ni kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya chama yanayoamuliwa na kupitishwa na vikao halali vya chama..!!

Sasa hao wanachama na wajumbe wa vikao hivyo wamulaumu kwa lipi wakati anatekeleza walichoamua??

Au unaamua kutufanya wajinga wasomaji wako??
 
Back
Top Bottom