TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Kwa akili hizo bora uendelee kujifukiza na gwajima
 
Kwenye taarifa za ukweli watu wameacha kufa??? .....USA, ITALY,UK, SPAIN......nk. wanakufa tu.
 
Mamabo leo anasemaje uko dar kwa hili tatizo au yupo askofu
 
Mitano tena. Sipati picha ikifika kwenye ule mwili wa Pole-slow si atakufa in 24 hrs?

Mkuu pamoja na tofauti, vizuri tusiombeane vifo.

Wote tutakufa ila tujitahidi kuishi kwa amani, ukweli, uadilifu, uaminifu, kutenda haki, kusaidia wenzetu, usawa.

Ongea ukweli bila matusi, dharau, kejeli.

Tunaweza tukauwawa, ila tukasaidia vizazi vijao, kama kuna Mungu tusiogope sana kifo.

This is temporary life, we will all submit our accounts to God.
 
Na nyie fanyeni kitu sio kukariri maandishi tu, sijui shule mlienda kusoma nini?? Kweny ishu serious za kutafuta chanjo mpo kmy poor Wasomi wa Tanzania

Point is?

Chanjo zote hutafutwa na sio mtu mmoja, ni Combined effort which need serious funding.

Labda tuungane na Cuba.
 
Kwa akili hizo bora uendelee kujifukiza na gwajima


Sio kwamba najifukiza tu, barakoa navaa na sasa hivi nimeongeza ‘star aniseed’ kwenye mchemsho wangu wa limau, asali na tangawizi.

Hapo ujaona dua zangu, halafu mimi sasa COVID niliipata tangu mwaka jana mpaka leo mapafu hayapo sawa. Kuna wengine ina wa affect vibaya, asilimia kubwa ya wazungu wazee waliokufa kipindi cha December 2020 ni wale waliopata mapema mwaka jana kwenye first wave na kupona baada ya matibabu, only COVID kuamka tena December (kwa ivyo si kweli ukipata mara moja ukapona, upati tena).

Usichezee na COVID kama wewe immune system yako tia maji tia maji.
 

Huyo kahaba hakuna anachochangia humu yeye kazi yake ni kupotosha tu achana naye. Si bure ni mtu mzima ana familia
 
Hebu acha kujitoa ufahamu wewe! Umemuona Biden na VP wake wanavaa barakoa katika Serikali hii ni yupi anayevaa barakoa? Sababu za kutovaa ni zipi?
Kwenye taarifa za ukweli watu wameacha kufa??? .....USA, ITALY,UK, SPAIN......nk. wanakufa tu.
 
Uko sawa Mkuu lakini hata 2020 hakuna ushahidi wa kutosha kwamba hakuna aliyekufa kwa corona. Nadhani hii ilikuwa ni baada ya vifo vya Mama Lwakatare na Mahiga.
Mkuu BAK katika yote ninazidi kuumia sana. Hizi ni sacrifices or kafara au? Uchungu hakuna? Many are fighting for their lives yet we are fucked. Yaani sijui nisamehe.
 
Uko sawa kabisa Mkuu nchi inapokuwa na pengo la uongozi matokeo yake ndiyo haya sasa maana hata uongo una mipaka yake Mkuu.
Mkuu BAK katika yote ninazidi kuumia sana. Hizi ni sacrifices or kafara au? Uchungu hakuna? Many are fighting for their lives yet we are fucked. Yaani sijui nisamehe.
 
Sitaki kuamini kama kweli Rais Magufuli alitangaza kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John William Kijazi kwa masikitiko makubwa. Kusema ule ukweli kama kuna kitu kibaya ambacho Rais Magufuli amewatendea watanzania na diaspora ambao wamekuwa wakim-support ni ukaidi wake wa kutotaka kuamini kuwa virusi wa Corona ni virusi hatari sana na siyo kitu cha kukilalia mlango wazi.

Rais Magufuli katika kukabiliana na janga la Covid 19 hapa Mzee hukucheza karata nzuri. Naomba kuanzia leo utambue kuwa wewe ni PHD-holder katika Chemistry, haimaanishi kuwa wewe pia ni mtaalam wa mambo ya Virus na mengineyo yanayo husu afya za binadam. Mambo kama haya ulitakiwa kuwaachia wenyewe walio bobea. Katika ku-handle hili janga umechemsha Mzee na ume act kama Ras Donald Trump kwa namna alivyo mbana koo Dr. Fauci. Umefanya kitendo cha kusikitisha sana Rais wangu kwabana koo madoktor wako.

Kwenye wimbi hili la pili la Coronavirus, hakuna mtu alitaka kukushauri eti uweke Lockdown, no, hiyo haikuwa issue. Kilicho takiwa Rais wangu ni kuwatahadharisha watanzania kuwa wawe makini na waangalifu katika mikusanyiko. Na vile viele kuangalia kuwa wagen na watanzania wanaoingia kutoka nje na hasa wale wanaotoka nchi ambazo zina maambukizi makubwa kama Uerope na South Africa kuchukua tahadhari za hali ya juu.

Watu wengi sana walikushauri kulinda mipaka, yaani kuilinda mipaka kwa kuweka High tech Equipment ambayo iko accurate katika kupima Covid 19 kwa haraka na kutoa majibu kwa haraka.

Sikatai kuwa unataka kuyaona maendeleo ya watanzania, lakini kama kitu hakiwezekani kubaliana nacho na jitahidi kuepusha madhara makubwa yasitokee. Halafu kitu kingine Rais wangu, naonba ujifunze kufanya vitu kwa manufaa yako na ya wananchi wako na sio kwa ajili ya kuuonyesha ulimwengu kuwa wewe ni zaidi. Haiendi hivyo. Ukilazimisha mambonmatikeo yake ndiyo unayaona kama haya yaliyo kutokea ya kimpoteza mtendaji kazi wako wa moyoni.

Umeambulia nini? Mimi naona umepata set back! Na sidhani kama utakuwa na moyo uleule wa kuendelea kuwaletea maendeleo watanzania kama ukivyo tarajia. Nimeshangaa sana kuona Rais intelligent kama wewe amnaye umethubutu mambo makubwa na mazito, unaanguka kwenye kitu kidogo kama huu ugonjwa wa Civid 19. Ulikuwa na mda mrefu wa kujiandaa na wimbi la pili badala yake ulikakamaa na kuling'ang'ania vitu ambavyo vilijulikana fika kuwa unacheza na wakati.

Huyo Mungu ni mungu gani atupende sisi watanzania tu na kuwaacha binadam wengine wote wateketee wakati huyo mungu mwenyewe ameletwa na meli na wamisionari waliotumwa na serikali za kufalme kutika Ulaya kuja kutuharibia dignity yetu. Ni kichekesho kikubwa!

Any way, ningekuomba sasa pamoja na mungu wako aliyeletwa na wazungu kujipanga upya kupunguza madhara makubwa zaidi yasiendelee kutokea. Sisi bado tuna kuoenda Rais wetu na tunakutakia mafanikio mema, lakini kwa hivi sasa kazania kiimarisha afya na maisha ya watanzania badala ya kuwaza maendeleo tu.

Kama unaona mda hautoshi kuweza kutimiza malengo yako, hilo lisikuoe shida, watanzania wengi wetu tulo tayari kulishauri bubge lako letu tukufu kukuongezea mda wa miaka mitanonzaidi ili ukamilishe uliyo yakusudia.

Tumia uwezo wako na waache wabobezi wakushauri na kukusaidia katika hatua unazotakiwa kuzichukua ili kulikabili hili janga. Wewe sio mungu na peke yako hutaweza kamwe kufikia mafanikio unayo yataka na kuyatarajia. Teamwork na watendaji wako ni kitu cha busara sana kulikabili hili janga. Usiwaache watanzania na watendaji wako wakapukutika kama majani ya mti kwa kujiona wewe ni Rais. Hata Rais ni binadam kama binadam wengine wote wliotokana na nyama na damu!

Usione haibu toka hadharani na kili kwa wazanzania kuwa ulilosea na hivi sasa utayaweka mambo kwenye mkondo unao husika. "Viel Glück mein President!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…