TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

TANZIA Katibu Mkuu Kiongozi, John W. Kijazi afariki dunia

Kumekucha!!! Hatimae mdudu ametia timu kwenye ofisi ya Mh Rais rasmi!!!

Kocha Magu ajipange apangike kweli kweli, mpaka ikifikia mwezi wa 4 hivi, atakua ameshapoteza "BENCHI LAKE LOTE LA UFUNDI MPAKA SUB ZOTE" kutokana na ule ugonjwa wa kishetani aliosema haupo Tanzania.

Itakua yeye "ANAFANYA UTEUZI" na Sir God nae "ANAFUTA UTEUZI". Kasheshe, Tutaongea lugha moja mwaka huu walai!!!

Mtu unalala huku una mawazo kilo 7 kichwani, mawazo ya kesho sijui utaamshwa na taarifa gani. Ukisikia simu inaita asubuhi asubuhi PRESHA INAPANDA kabla hata ya kupokea, roho ipo juu juu huna amani masaa yote. Ukiingia JF unakuta thread tatu tatu za misiba hujui uanze ku comment ipi!!!
Sir God anaeza mteua akaongoze malaika.
 
Nachojua mimi kwenye ufugaji chanjo huanza kabla ya ugonjwa.

Ukiwapa kuku chanjo ya mdonde kipindi ugonjwa umeingia utawamaliza kuku wote.

Sasa watz tukikubali chanjo tutegemee vifo vingi kisha hali itatulia maana mdudu keshakolea miongoni mwetu ila miili inajitahidi kujilinda.
 
Hii corona ya saiv kiboko.kirusi hiki kasi yake 5G...kinafyeka si masihara
 
Huwezi kuikataa adhabu ya Mungu kwamba haipo wakati Mungu ameamua kuishusha kisha Taifa la
Ikabaki.salama.

Rais wangu kukubali korona.ipo.na.kuwapima watu wako ili kujua ukubwa wa tatizo NI moja ya uwajibikaji wako kwa watu wako.
Nchi imevamiwa na adui ,ana silaha kubwa ,na za kisasa.

Badala ya kutoa jeshi lipambane kuwakoa watu wako, wewe unawaambia kila mwananchi achukue time , panga mkuki , kiujumla.silaha za jadi ili kukabiriana na adui! Huu siyo uamuzi wa Rais makini ,bali Rais aliyeshindwa na ambaye amepoteza uhalali wa kuwa Rais.

Tafakari Rais wangu
 
Mkuu sidhani kama hilo litatokea huyo anayejiita mwendawazimu na anayejua kila kitu duniani atuombe radhi Watanzania kwa kusema uongo na kuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa kusambaa kwa kasi kubwa na kusababisha maambukizi kusambaa kwa kasi kubwa na vifo kuwa vingi.

Imagine kama angehamasisha uvaaji wa barakoa nchini na kuepuka misongamano.




..Raisi na Waziri wa Afya wajitokeze na kuwaomba radhi wananchi.


..watu wanakufa kutokana na taarifa potofu walizopewa na viongozi kwamba covid19 si ugonjwa hatari.
 
Unaelewa wajibu wa serikali kulinda raia wake kwa kutoa taarifa, kuhamasisha,chanjo na kuwatibu?
Unapoona mtu mkubwa kama Rais wa marekani anasisitiza kila siku raia wake wavae barakoa na wachukue taadhari zote unadhani yeye ni zoba anayepoteza muda tu?
Kuchukua tahadhari hadi uambiwe na serikali? Are u serious?
 
Back
Top Bottom