Rais Magufuli ametangaza kwa masikitiko kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John William Kijazi ambaye amefariki leo Februari 17 saa tatu usiku, Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma akipatiwa matibabu.
WASIFU WA BALOZI JOHN KIJAZI >
Wasifu wa Katibu Mkuu Kiongozi mpya Balozi Mhandisi John William Kijazi
CURRICULUM VITAE
NAME: John William Herbert Kijazi
BORN: 18 November 1956
MARITAL STATUS: Married
CHILDREN: Has three sons
EDUCATION
- Bachelor of Science (Honours) in Civil Engineering, University of Dar es Salaam, Tanzania
- Masters of Science in Highway Engineering, Birmingham University, UK
CAREER
- 1982 – 1986 Assistant Executiver Engineer, Ministry of Public Works, Tanzania
- 1986 – 1996 Regional Engineer, Ministry of Public Works, Tanzania
- 1996 – 1999 Senior Road Maintenance Engineer, Ministry of Public Works, Tanzania
- 1999 – 2002 Director of Regional Roads, Ministry of Public Works, Tanzania
- 2002 – 2005 Permanent Secretary, Ministry of Public Works, Tanzania
- Jan – Nov 2006 Permanent Secretary, Ministry of Infrastructure Development, Tanzania
- Dec 2006 – Jun 2007 Special Duties, Minstry of Foreign Affairs and International Cooperation HQTS, Tanzania
- Jun 2007 High Commissioner to India
- 27 May 2013 High Commissioner to Singapore
LANGUAGES
English, Swahili
Sitaki kuamini kama kweli Rais Magufuli alitangaza kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John William Kijazi kwa masikitiko makubwa. Kusema ule ukweli kama kuna kitu kibaya ambacho Rais Magufuli amewatendea watanzania na diaspora ambao wamekuwa wakim-support ni ukaidi wake wa kutotaka kuamini kuwa virusi wa Corona ni virusi hatari sana na siyo kitu cha kukilalia mlango wazi.
Rais Magufuli katika kukabiliana na janga la Covid 19 hapa Mzee hukucheza karata nzuri. Naomba kuanzia leo utambue kuwa wewe ni PHD-holder katika Chemistry, haimaanishi kuwa wewe pia ni mtaalam wa mambo ya Virus na mengineyo yanayo husu afya za binadam. Mambo kama haya ulitakiwa kuwaachia wenyewe walio bobea. Katika ku-handle hili janga umechemsha Mzee na ume act kama Ras Donald Trump kwa namna alivyo mbana koo Dr. Fauci. Umefanya kitendo cha kusikitisha sana Rais wangu kwabana koo madoktor wako.
Kwenye wimbi hili la pili la Coronavirus, hakuna mtu alitaka kukushauri eti uweke Lockdown, no, hiyo haikuwa issue. Kilicho takiwa Rais wangu ni kuwatahadharisha watanzania kuwa wawe makini na waangalifu katika mikusanyiko. Na vile viele kuangalia kuwa wagen na watanzania wanaoingia kutoka nje na hasa wale wanaotoka nchi ambazo zina maambukizi makubwa kama Uerope na South Africa kuchukua tahadhari za hali ya juu.
Watu wengi sana walikushauri kulinda mipaka, yaani kuilinda mipaka kwa kuweka High tech Equipment ambayo iko accurate katika kupima Covid 19 kwa haraka na kutoa majibu kwa haraka.
Sikatai kuwa unataka kuyaona maendeleo ya watanzania, lakini kama kitu hakiwezekani kubaliana nacho na jitahidi kuepusha madhara makubwa yasitokee. Halafu kitu kingine Rais wangu, naonba ujifunze kufanya vitu kwa manufaa yako na ya wananchi wako na sio kwa ajili ya kuuonyesha ulimwengu kuwa wewe ni zaidi. Haiendi hivyo. Ukilazimisha mambonmatikeo yake ndiyo unayaona kama haya yaliyo kutokea ya kimpoteza mtendaji kazi wako wa moyoni.
Umeambulia nini? Mimi naona umepata set back! Na sidhani kama utakuwa na moyo uleule wa kuendelea kuwaletea maendeleo watanzania kama ukivyo tarajia. Nimeshangaa sana kuona Rais intelligent kama wewe amnaye umethubutu mambo makubwa na mazito, unaanguka kwenye kitu kidogo kama huu ugonjwa wa Civid 19. Ulikuwa na mda mrefu wa kujiandaa na wimbi la pili badala yake ulikakamaa na kuling'ang'ania vitu ambavyo vilijulikana fika kuwa unacheza na wakati.
Huyo Mungu ni mungu gani atupende sisi watanzania tu na kuwaacha binadam wengine wote wateketee wakati huyo mungu mwenyewe ameletwa na meli na wamisionari waliotumwa na serikali za kufalme kutika Ulaya kuja kutuharibia dignity yetu. Ni kichekesho kikubwa!
Any way, ningekuomba sasa pamoja na mungu wako aliyeletwa na wazungu kujipanga upya kupunguza madhara makubwa zaidi yasiendelee kutokea. Sisi bado tuna kuoenda Rais wetu na tunakutakia mafanikio mema, lakini kwa hivi sasa kazania kiimarisha afya na maisha ya watanzania badala ya kuwaza maendeleo tu.
Kama unaona mda hautoshi kuweza kutimiza malengo yako, hilo lisikuoe shida, watanzania wengi wetu tulo tayari kulishauri bubge lako letu tukufu kukuongezea mda wa miaka mitanonzaidi ili ukamilishe uliyo yakusudia.
Tumia uwezo wako na waache wabobezi wakushauri na kukusaidia katika hatua unazotakiwa kuzichukua ili kulikabili hili janga. Wewe sio mungu na peke yako hutaweza kamwe kufikia mafanikio unayo yataka na kuyatarajia. Teamwork na watendaji wako ni kitu cha busara sana kulikabili hili janga. Usiwaache watanzania na watendaji wako wakapukutika kama majani ya mti kwa kujiona wewe ni Rais. Hata Rais ni binadam kama binadam wengine wote wliotokana na nyama na damu!
Usione haibu toka hadharani na kili kwa wazanzania kuwa ulilosea na hivi sasa utayaweka mambo kwenye mkondo unao husika. "Viel Glück mein President!"