msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 929
- 1,764
Badala ya kutoa majibu yanayo eleweka umeishia kujichanganya huku ukijibu kisiasa zaidi kwa kujikanyaga kanyaga
Umesema mmetii agizo la mheshimiwa Rais la kuajiri walimu 13000 hapo hapo unasema mmeajiri walimu 8000 katika awamu ya kwanza. Hata hao elfu 8 hawajafika. wengine wapatao 5000 ukasema watajiriwa awamu nyingine ya pili.
Sababu za kutoa kwa awamu ndio vichekesho mara useme zingine zitafuata baada ya hatua nyingine kukamilika mara mmetoa kwa awamu kupunguza malimbikizo ya mishahara. Hapo hapo unadakia mmetoa fursa ili changamoto zilizo jitokeza kwenye mfumo zifanyiwe marekebisho ndipo mtoe ajira zingine. Kiufupi hujaeleweka kabisa
Kwani ungesema ukweli kwamba serikali haina hela za kuajiri wote kwa mkupuo ungepungiwa nini?
Hivi hayo ndio yalikuwa maagizo ya Rais kwamba muajiri kwa awamu?
Mzee bora ungenyamaza kuliko kuwalaghai vijana maana hata body language yako inaashiria wazi kuwa serikali haina hela. Hata hayo majibu umetoa kisiasa zaidi ili kuwapa moyo vijana waliokosa lakini yamejaa chembe chembe za uongo na ulaghai kwa vijana