Nina Jambo moja tu kuhusu TAMISEMI,UTUMISHI (na MOEVT);
Hivi unamuajiri mwalimu aliyehitimu chuo mwaka2019,unamuacha yule aliyehitimu mwaka 2016 una maanisha nini?
Kwa kawaida aliyehitimu chuo mwaka 2016 ana umri mkubwa kuliko yule aliyehitimu mwaka 2019(roughly). Sasa hamuoni kwamba Kuna uwezekano mkubwa wa huyu wa mwaka 2016 aidha kuzeeka bila kuajiriwa au kuajiriwa akiwa mzee.Sijui wataalam kutoka TAMISEMI,UTUMISHI(na MOEVT)wanaliona hili kwa jicho la ki-zalendo.
MAONI YANGU: Pamoja na vigezo vyote mnavyojinasibu navyo,mzingatie sana suala la umri wa waombaji,hata Kama wamehitimu hivi karibuni. Mnawakosesha heshima walimu wenye umri mkubwa na waliohitimu miaka mingi iliyopita.