AnasemaKatibu Mkuu wa Chama cha NRA, Hassan Kisabya, ametoa kauli kuhusu madai ya utekaji nchini wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kisabya alidai kuwa baadhi ya watu wanatumia madai ya kutekwa kwa malengo ya kuchafua taswira ya nchi. Pia alihimiza kuondoa mtazamo wa kisiasa kama ugomvi, akisisitiza umuhimu wa mijadala yenye kujenga badala ya kugawanya taifa.
-kwamba siasa si ugonvi
-kwamba si sahihi kutumia utekaji kuchafua taswira ya nchi
Huyu anatambuwa kuwa upo utekaji/mauaji ktk jina la siasa, kwanini aseme siasa si ugonvi wakati kuna waliouliwa, kupotezwa, kujeruhiwa kwasababu ya siasa?.
Anayechafua taswira ya nchi ni mtekaji na si anayezungumzia matukio ya utekaji.