Katibu Mkuu TFF na Msemaji wa Yanga warushiana maneno mazito na ya kashfa Clouds fm

Huyu
Haya yanarudiwa tu hapa mkuu. Tumemsikia msemaji wa yanga kwenye kipindi cha sports round up cha kila jumapili kiukweli kaonyesha umbumbumbu wa hali ya juu. Alikua anaongelea akibishana bila ustaarabu. Alikua hajibu hoja bali alitaka wakubaliane na anachokielewa wewe.. Kiukweli nimeshindwa kufaid kipindi cha leo Kwa sababu ya upuuzi alokua anaongea huyu jamaa. Kuna mda aridiriki kusema yanga ni zaid ya CAF. There is something wrong with this guy
 

Kwenye red hizo za mwisho mwisho umeweka 'unazi' au 'ushabiki' wako jambo ambalo siyo zuri. hujawa objective kwa habari hii...hata hivyo pamoja na hayo, naisikitikia sana YANGA...sina comments zaidi...
 


YANGA iko matatizoni, Umaskini ndio unaoitesa YANGA, ni umaskini wa pesa na uelewa...Hofu yangu ya dhati kwa YANGA ni kutokea yale yaliyotokea mwaka 1975/76 ambapo YANGA ilisambaratika na kuzaa Nyota ya Morogoro na baadaye PAN AFRICAN ....
 
Kama akiwa ni yeye au si yeye Wewe utafaidika na nini? Na labda ukishamjua umasikini wako wa akili na mali ndiyo utakwisha au?
pole Sana inaonekana muro anakuumiza Sana kichwa sijui unatamani nafasi yake au la,hakuna siku inakupita bila kumuwaza huyu jamaa.hao clouds fm wamemualika ila kumpa nafasi ya kuongea hamna shaffih kila saa anaingilia yote hujayaona.nashawishika kuamini kuwa Una chuki zaidi na Jerry muro
 
Kwa hatua mliyofikia, hata siku akisema yanga tunataka kucheza mechi uchi, mtamshangilia tu! hii ni aina ya ushabiki wa kipumbavu tuliyofikia. Ndiyo maana tusapoti hata upumbavu! Mtaalam wa CAF amefafanua kila kitu, lakini mtu bado anatoa povu! Sijui tatizo ni lugha?!
 

Kama na wewe unawanafunzi basi wako katika hasara na unataka wawe watiifu? itakuwa sio UDSM haki ya mungu. Jerry yuko sahihi simamia katika haki na ukweli CAF si ndio hawa wana chaguaga raisi wa FIFA kwa kulazimisha misaada mamelody sundowns ilileta team B kwa Azam sababu walisema ligi ya SA ni bora kuliko kombe la washindi. Akina SHafih daduda wanapenda safari hawawezi kuwa na msaada kwa yanga. Yanga lazima wajisemee ile wanayoona inafaa kwa maslahi yao, mikataba ya CAF ni Zaidi ya ukoloni.
 
Anawaharibia wanayanga kama anataka mipasho aombe kipindi naye warumbane kwa mada yao ya Mani msomi kuliko mwenzake waweke kando kazi zao maana wanatutia kichefuchefu kwani ni viongozi
 
Watanzania tujizoeshe tabia ya kukaa kimya zinapokuja thread za kipumbavu kama hizi,nawapa taarifa tu ndugu zangu.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka sana mkuu
 

Akhsante kwa kuja.
 

Safi sana Mkuu ila usisahau pia kuwa Yanga ndiyo timu pekee hapa duniani inayoongoza kuwa na " vilaza " waliotukuka wengi huku Simba ikiwa katika top 5 ya Klabu yenye intellectuals wengi. Jerry Muro anawakilisha AKILI na UPEO wa Wana Yanga wote duniani kwa 100%.
 
Kitu cha muhimu ni kushinda mechi ya kesho mengine yatapita kama upepo
 
fuatilieni na
Mzee akilimali aliyoyasema,ndo mjue jery muro aliyoyaongea yaana ukweli kiasi gani, bila kupepesha macho Tff ndo tatizo kubwa , yanga wanaposema haki za matangazo tff wameuza ,ni kweli why only Azam TV? wakati ilitakiwa wawe TBC
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…