Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu akamatwa na Polisi usiku wa manane

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu akamatwa na Polisi usiku wa manane

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
643
Reaction score
1,603
Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Ado Shaibu Ado amekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani Tunduru jana Agosti 27 2020 saa sita usiku.

Askari Polisi Wilayani Tunduru wakiongozwa na Mkuu wa Kituo (OCD) wakiwa na silaha za moto walimfuata Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu nyumbani kwake Mtaa wa Kalanje, Tunduru na kumuamuru wafuatane naye hadi kituo Cha Polisi Tunduru kwa kile walichodai kuwa ni suala la kulitolea ufafanuzi

Baada ya kufika kituoni OCD alimweleza Katibu Mkuu ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kuwa gari lake linasemekana limeteka watu kijijini Malombe.

Hata hivyo, baada ya OCD kuelezwa kuwa gari hilo lilibeba viongozi na wanachama wetu alilazimika kumuachia Ndugu Ado na kumtaka kurejea leo asubuhi, Agosti 28, 2020 kwa mahojiano zaidi.
Gari la Ndugu Ado ambalo lilikaguliwa na kukutwa na bendera za chama pekee, linaendelea kushikiliwa Polisi.

ACT-Wazalendo tunapenda kuutaarifu umma wa Watanzania kuwa huu ni mwendelezo wa matukio ya kumuandama Ndugu Ado katika Jimbo la Tunduru Kaskazini kwa kuratibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoogopa ushindani wa wazi nawa kidemokrasia.

Wakati hayo yakiendelea, mapema jana tarehe 27 Agosti (saa 4 asubuhi) Ndugu Ado aliitwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tunduru kuwa kuna pingamizi dhidi yake.

Ndugu Ado alipohoji kuwa mbona hadi saa 10.00 muda wa mapingamizi ulipofika mwisho CCM walikuwa hawajaweka pingamizi lolote na kwa nini apokee pingamizi nje ya muda, Msimamizi wa Uchaguzi aling'ang'ania kuwa pingamizi hilo lilikatwa kwa wakati.

Chama cha ACT- Wazalendo tumebaini pasipo shaka kwamba, mpango uliopo chini ya uratibu wa CCM wilayani Tunduru ni kuwaengua wagombea wetu wawili, Ndugu Ado Shaibu Ado (Tunduru Kaskazini) na Mtutura Abdallah Mtutura (Tunduru Kusini) pamoja na wapinzani wengine ili CCM ipite bila kupingwa.

Kwa msingi huo tunalitaka Jeshi la Polisi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inayoongozwa na Jaji Semistocles Kaijage watoe maelekezo na kumuonya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tunduru na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutenda haki na kuwaacha Wanatunduru Kaskazini na Kusini na kwingineko wachague wawakilishi wanaowapenda.

Janeth Rithe
N/Katibu wa Uenezi, Habari na Mahusiano kwa Umma

ACT Wazalendo Taifa

28 Agosti 2020

IMG_20200828_094937.jpg
 
OCD wa Tunduma asomewe Albadiri haraka iwezekanavyo na huyo Silinde ajiandae kuwa mbunge zezeta kwani huo upumbavu wake asifikiri ataishi Dodoma miaka yote
 
Tumejitahidi kukwepa tunakopelekwa na viongozi hawa wenye kufuata maelekezo ya kidhalimu ili wafanikishe azma mbaya ya CCM ipite bila kupingwa, ila naona uvumilivu umefika mwisho.
 
Usiku wa manane anatafuta nini? Huo ni muda hatari sana kiusalama wa binadamu, isije kuta ni jambanoko huyu jamaa
 
OCD wa Tunduma asomewe Albadiri haraka iwezekanavyo na huyo Silinde ajiandae kuwa mbunge zezeta kwani huo upumbavu wake asifikiri ataishi Dodoma miaka yote
Silinde ameingiaje hapa tena?
 
OCD wa Tunduma asomewe Albadiri haraka iwezekanavyo na huyo Silinde ajiandae kuwa mbunge zezeta kwani huo upumbavu wake asifikiri ataishi Dodoma miaka yote

Mkuu tunduma tena! Duh minyoo imekimbilia kichwani eee.
 
Kufanya siasa za Upinzani Tanzania ni hatari kuliko kuwinda Nyati. Yaani muda wowote ule kesho yako huijui - unaweza kuwa sadaka at any time

Wale wazee wawili wa CCM walikwenda upinzani wee amejisalimisha wenyewe !! Mmoja katishwa na mwengine wakachukua mashamba yake yote balaaa.
 
Kufanya siasa za Upinzani Tanzania ni hatari kuliko kuwinda Nyati. Yaani muda wowote ule kesho yako huijui - unaweza kuwa sadaka at any time t. ..

Wale wazee wawili wa CCM walikwenda upinzani wee amejisalimisha wenyewe !! Mmoja katishwa na mwengine wakachukua mashamba yake yote balaaa.
Dahh acha tu, ninaamini usemi wa Mbowe kwamba kuwa mpinzani Tanzania lazima uwe na ngozi ngumu.
 
OCD wa Tunduma yafaa afikishwe kwenye mahakama ya uhalifu The Hague mara moja kwani sasa amezidi unyanyasaji kuwabambikia kesi kwa kiwango cha kutisha zaidi
Huko tunakoelekea tunaenda kuwa nchi inayoendekeza siasa za kishamba zaidi duniani!!! Na cha ajabu watu wanahimiza amani bila kwanza kuanza na HAKI!!!
 
OCD wa Tunduma asomewe Albadiri haraka iwezekanavyo na huyo Silinde ajiandae kuwa mbunge zezeta kwani huo upumbavu wake asifikiri ataishi Dodoma miaka yote
Mitandao ni hatari; yaani makurupukaji yamejazana kibao. Mleta mada anaongelea swala la Tunduru, jitu moja lisilo soma linakurupuka na Tunduma + Silinde.
 
SGR, Stielgers gorge, Ndege, Fulahi ova, mabarabara vyote hivyo hamuwezi kuvinadi kwa watanzania hadi mtumie polisi kupata ushindi? CCM nani kawaloga
 
Mtutura Abdalah alikuwa Mbunge kupitia CCM baada ya kifo cha Mbunge na Waziri Hayati Jamaldeen Akukweti kumbe nae kajiunga Chama cha Hizb?
 
TAARIFA:

KATIBU MKUU WA ACT WAZALENDO AKAMATWA NA POLISI USIKU MNENE, MSIMAMIZI UCHAGUZI TUNDURU AANZA FIGISU

Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Ndugu Ado Shaibu Ado amekamatwa na Jeshi la Polisi Wilayani Tunduru jana Agosti 27 2020 saa sita usiku.

Askari Polisi Wilayani Tunduru wakiongozwa na Mkuu wa Kituo (OCD) wakiwa na silaha za moto walimfuata Katibu Mkuu Ndugu Ado Shaibu nyumbani kwake Mtaa wa Kalanje, Tunduru na kumuamuru wafuatane naye hadi kituo Cha Polisi Tunduru kwa kile walichodai kuwa ni suala la kulitolea ufafanuzi.

Baada ya kufika kituoni OCD alimweleza Katibu Mkuu ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kuwa gari lake linasemekana limeteka watu kijijini Malombe.

Hata hivyo, baada ya OCD kuelezwa kuwa gari hilo lilibeba viongozi na wanachama wetu alilazimika kumuachia Ndugu Ado na kumtaka kurejea leo asubuhi, Agosti 28, 2020 kwa mahojiano zaidi.

Gari la Ndugu Ado ambalo lilikaguliwa na kukutwa na bendera za chama pekee, linaendelea kushikiliwa Polisi.

ACT-Wazalendo tunapenda kuuarifu umma wa Watanzania kuwa huu ni mwendelezo wa matukio ya kumuandama Ndugu Ado katika Jimbo la Tunduru Kaskazini kwa kuratibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoogopa ushindani wa wazi na wa kidemokrasia.

Wakati hayo yakiendelea, mapema jana tarehe 27 Agosti (saa 4 asubuhi) Ndugu Ado aliitwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Tunduru kuwa kuna pingamizi dhidi yake.

Ndugu Ado alipohoji kuwa mbona hadi saa 10:00 jioni muda wa mapingamizi ulipofika mwisho CCM walikuwa hawajaweka pingamizi lolote na kwa nini apokee pingamizi nje ya muda, Msimamizi wa Uchaguzi aling'ang'ania kuwa pingamizi hilo lilikatwa kwa wakati.

Chama cha ACT- Wazalendo tumebaini pasipo shaka kwamba, mpango uliopo chini ya uratibu wa CCM wilayani Tunduru ni kuwaengua wagombea wetu wawili, Ndugu Ado Shaibu Ado (Tunduru Kaskazini) na Mtutura Abdallah Mtutura (Tunduru Kusini) pamoja na wapinzani wengine ili CCM ipite bila kupingwa.

Kwa msingi huo tunalitaka Jeshi la Polisi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inayoongozwa na Jaji Semistocles Kaijage watoe maelekezo na kumuonya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tunduru na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutenda haki na kuwaacha Wanatunduru Kaskazini na Kusini na kwingineko wachague wawakilishi wanaowapenda.

Janeth Rithe, N/Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano, ACT Wazalendo.
28 Agosti 2020.
 
Back
Top Bottom