Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
CCM ILITELEZA HAPA, IKAANGUKIA HAPA...!
Nimemsikiliza Dr.Emmanue Nchimbi kwa zaidi ya mara tano kwa utulivu mkubwa sana.
CCM naijua lakini Dr. Emmanuel Nchimbi namfahamu vizuri sana. Binafsi sioni ghilba wala ulaghai nikitazama “demeanour” yake na facial expression yake haina chembe ya uongo.
Ujumbe pekee ambao naona Dr. Emmanuel Nchimbi ametaka Dunia na Watanzania waupate kwa lugha fiche.
Dr.Emmanuel Nchimbi anajaribu kuiambia Dunia kuwa
1.CCM haifanyi utekaji na haikubaliani na Magenge ya utekaji
2.CCM haina nguvu wala maarifa ya kupambana na magenge ya utekaji.
pamoja ya kwamba wao ndiyo wenye dhamana ya kutulinda watanzania na mali zetu pamoja na mipaka ya nchi yetu
Mimi nipo tayari kuwapa dawa CCM kwa sharti la kupanua mdomo bila kuwakaba mikono na kuwabana pua kwa kuwapa ukweli huu ufuatao.
1.Uteuzi wa IGP Camillus Mongoso Wambura
Hili lilikuwa ni kosa kubwa sana katika historia ya Jeshi la Polisi na historia ya Tanzania. Wakati Dunia ya Sasa inateua IGP kwa elimu, maarifa, ujuzi wake ndani ya Jeshi la Polisi pamoja na ushiriki wake wa mafunzo na ushiriki wake katika Interpol kama ilivyokuwa kwa IGP Said Mwema au IGP Ernest mangu
IGP wetu huwezi kupata rekodi yake ya taaluma yq ubobevu wa Juu zaidi ya histori yake ya madaraka.
Majirani zetu wote utaona Ma IGP wao rekodi zinaonyesha walisoma Federal beural of investigations at national executive Institute kule Fredericksburg, Virginia,USA au wamesoma Intensive course for high school security management at the professional school of security PSOS,Tel-Aviv,Israel au Vyuovikuu vya Mapolisi wabobevu Duniani.
CCM mlimteua IGP Camillius Wambura kwa kigezo cha ushiriki wake wa Operesheni ya MKIRU (Mkuranga, Kibiti Rufiji) na kazi zake alizofanya akiwa Zonal Crime Officer (ZCO) wa Kanda Maalum ya Dar es saalam kwa kutengeneza Vikosi kazi (Task force) za kuendesha Operesheni za siri za kukabiliana na uhalifu kwa kutumia njia ya uhalifu akiwa Mkuu wa Operesheni za Polisi Makao makuu.
Leo mnashangaa magenge ya utekaji yametoka wapi? Mnachekesha sana.
2.Uteuzi wa DCI Ramadhani Kingai
Wakati Dunia ya Sasa inateua ma DCI kwa Ujuzi wao wa Juu wa sheria na na utekelezaji wa sheria.
Mtu ambaye ana mafunzo ya kimataifa ya kupambana na makosa ya Jinai kwa kutumia tecknolojia za kisasa namna ya kubaliana jinai zinazotokana na akili bandia (AI)
Majirani zetu utaona DCI anaonekana rekodi yake ya taaluma ya ubobevu wa uchunguzi kwa kusomea Policing and Terrorism in Democratic societies course pale the international Faculty Bramshil ya Centrex police College,United Kingdom
Amin Mohamed Ibrahim DCI wa Kenya ana taaluma ya Banking fraud investigations,ana masters ya criminology na security studies (first class honors) kutoka chuo cha Egerton Uingereza,Diploma ya international studies,cheti cha National Defense College and ethics cheti cha Economic crimes kutoka Chuokikuu cha Egerton.
CCM mliteua Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI Ramadhani Kingai (DCI) kwa sifa na rekodi ya kupambana na wapinzani wa Serikali ya CCM na ujuzi wa kuwabambikia kesi za uongo wapinzani wenu kama ilivyokuwa kwa Freeman Mbowe.
Mmegawa cheo cha U-DCI kama zawadi kwa wapambe na makada wenu leo mnashangaa magenge ya utekaji yametoka wapi? au kwanini hayadhibitiwi.
3. Namna ya kupandisha vyeo Maafisa waandamizi wa Vyombo vya Dola.
Wakati Dunia inatumia mbinu za upembuzi wa kazi na matokeo chanya ya maafisa wa majeshi kwa nafasi wanazoshika katika utekelezaji wa majukumu yao kwa uwazi na kwa kuzingatia sheria.
CCM mnateua watu wa kuwashikisha adabu wapinzani wenu huku mkiwahaidi kuwalinda watakapovunja sheria na kufanya uhalifu.
Mkawasifia MaRCO wanaozuia uhalifu kwa kutenda uhalifu,
Mkafanya maafisa wengine wapolisi waone mafunzo ya ukachero kutoka pale Chuo cha Polisi Moshi-CCP hayana kazi na hayawezi kukusaidia kupanda cheo
Bali Ma RCO waliojua kuteka,kukamata,kupiga watuhumiwa risasi,Kuwafunga tape,Kuwafunga mifuko ya nailoni usoni na kisha kutupa miili ya watuhumiwa ndiyo wanaojua kazi ya upolisi.
Maafisa wa Polisi waliofuatisha na kuamini masomo yao ya Chuo cha Polisi Moshi- CCP ya kupambana na Wahalifu kwa kutumia Police General Orders -PGO,Criminal Procedures ACT na Penal Code (CAP.16 RE 2022) ni washamba na waoga.
CCM mkaziba masikio yenu wakati watanzania mamia walipo kuwa wanawatafuta ndugu zao katika vyumba vya kuhifadhia maiti huku wakikutwa na matobo ya risasi ndani ya majokofu ingali walichukuliwa majumbani kwa wazazi wao wakiwa wazima.
Leo na ninyi CCM mnaweza kweli kutoka hadharani kushangaa magenge ya utekaji yametoka wapi.?
4.Matamko ya Makada na Viongozi wa CCM yenye kuhamasisha utekaji na mauaji.
CCM hakutaka Viongozi wenu wanaotoa kauli za kuchochea utekaji na mauaji wakamatwe na kushtakiwa mahakamani. Mliwalinda.
Mlizuga kwa kujifanya mnakanusha kauli zao siyo kauli za CCM lakini tuliendelea kuwaona Mwenyekiti wa UVCCM kule Kagera na Spika wa Bunge JMT akitoa kauli za kuhamasisha watu wanaokinzana na Viongozi wa CCM kwa Mawazo washughulikiwe, ingali ni kinyume na Katiba na sheria za nchi.
5.CCM mkabadilisha Sheria ya Usalama wa Taifa, iruhusu kukamata watu mtaani bila uniforms, bila kujua mahabusu za wakamataji mahala zilipo
na mwisho mkaweka na vifungu vya kuwalinda watakao tenda uhalifu ndani ya Usalama wa Taifa kutoshitakiwa mahala popote.
Leo bila aibu na nyie CCM mnashangaa magenge ya uhalifu kama sisi wananchi.
6.kwanini Viongozi wa CCM hawatekwi wala Kupotea..?
Wanaotekwa ni Viongozi na Makada wa Upinzani pekee yake kama Dioniz Kipanya, Godwin Mlay, Deusdedith Soka na Frank Mbise na marehemu Ali Kibao.
CCM hawana nia ya dhati ya kukomesha utekaji kwa sababu hawajui machungu ya viongozi wao kutekwa na kupotea au kuokotwa wakiwa wamefariki vichakani.
CCM awamu hii hawajaguswa kabisa, kutekwa na kupotezwa.
7.CCM kushindwa kuwawajibisha viongozi wake wenye dhamana ya ulinzi na Usalama wa raia
Tufanye kweli CCM haiteki watu wala haiwajui wanaoteka watu. Je nini kinachowazuia CCM kuwawajibishwa viongozi wao wenye dhamana ya ulinzi na usalama wa raia wake.
Miaka ile iliwezekana kwa Rais Ally Hasaan Mwinyi kujiuzulu ili kuwajibika kwa mauaji ya vikongwe Kanda ya Ziwa pamoja na Viongozi wa vyombo vya Dola.
CCM hii Kibogoyo inapata wapi muda wakuja kulalamika kwetu wananchi ingali wanayo mamlaka ya kuwawajibisha Viongozi wao.
8.CCM kuendelea kuteua na kufanya kazi na watu wenye historia na rekodi ya ukatili na uhalifu kipindi cha awamu ya tano
Tumeanza Kuona baadhi ya Wakuu wa mikoa,Wakuu wa wilaya na hata aliyekuwa Mkuu wa Dawati la Siasa wakati wa Hayati Magufuli kurejeshwa katika nafasi ya Dawati la Siasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu. Hii siyo ishara njema.
Je CCM wanachoshangaa ni kipi? Kama wao wameenda Kukodi jeshi la Ukatili na kuwapa wajibu wa kufanya ukatili,
CCM wanashangaa nini wakiona ukatilili unarejea ghafla. Au wanatuchora tu?
10.Kigugumizi cha kuchukua hatua katika matukio ya ukatili yanayofanywa na maafisa wa Jeshi la Polisi au Viongozi wa vyombo vya dola.
Mfano mdogo ni sakata la Edger Edson Mwakabela (SATIVA) kutekwa ,kusarishwa na baadae kwenda Kupigwa risasi katika poti la hifadhi ya Taifa ya Katavi.
SATIVA tayari amemtambua hadharani mtesi wake, ACP Faustine Mafwele na Dunia inajua
lakini CCM wanajifanya hawaoni tuhuma za Sativa wala hawajawahi kuzisikia mahala popote.
Lakini leo CCM wanatoka hadharani kuja kutuomba wananchi na vyama vya Upinzani tuwatambue watekaji na wauaji.
Wapo serious au wanafanya utani na Maisha ya Watanzania.CCM acheni UTANI na MZAHA katika maisha ya watanzania.
Kwa lugha nyepesi ,ni kwamba CCM mmekuja msibani mnalia kama sisi ila tunashangaa kwanini hamtokwi na machozi kama sisi..?
Mnalia kweli au Mnatuchora..!
Happy Sabbath
Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
The voice of the silenced Majority.