Katibu Mkuu wa CCM, Dr. Emmanuel Nchimbi, jitokeze kujibu hoja hizi za Bonifa Jacob alizozitoa kupitia mtandao wa X

Maafisa wa Polisi waliofuatisha na kuamini masomo yao ya Chuo cha Polisi Moshi- CCP ya kupambana na Wahalifu kwa kutumia Police General Orders -PGO,Criminal Procedures ACT na Penal Code (CAP.16 RE 2022) ni washamba na waoga.
Luckydube anasema you stand aside and look while the Nation Cries.

Mungu atuokoe sana
 
CCM huwa wanashangaza sana...

Serikali ikitokea imefanya mambo mazuri kama ujenzi wa barabara, hospitali n.k basi kauli zao huwa ni kusifia chama chao, Rais n.k

Lakini sasa itokee kwamba serikali imeboronga, huwezi kuwasikia hata siku moja wakiwajibika wala kuendelea kujiita wao ni serikali au kumkemea Rais n.k.
 
Uzi umetulia sana
 
Sasa Bwashe inakuwaje mtu ambaye hana hofu ya Mungu hata chembe kama Ramadhani Kingai anakuwa DCI?! Kwa hiyo mamlaka inayoteua hao watu wenye rekodi ya uhalifu kama akina Bashite ndiyo tatizo zaidi. If yes, wananchi waifanyeje hiyo mamlaka ili iwe inateua watu wasio na rekodi ya uhalifu?
 
Kiufupi teuzi hazifanywi na CCM so hoja Haina mantiki.

Pili kusema kigezo Cha Polisi wa Tanzania kupata vyeo lazima wakasome Vyuo vya Nje ya Nchi ni aina nyingine ya ujinga ,mfano unaogopa wa Kenya huko Kenya Kuna Uhalifu mkubwa sana wa Polisi ikiwemo mauaji holela eg kwenye maandamano ya juzi nk.

Mwisho nakubalina na hoja ya Kwamba Kwa nini wanaotekwa ni Wapinzani tuu lakini sio ccm.

Pamoja na hii hoja ila aliyetakiwa kunyoshewa kidole ni Serikali na sio CCM kama chama.

Utekaji haukubaliki na pia sheria za kuwalinda Watekaji haikubaliki hususani pale watakapohusishwa na Serikali.
 
Viongozi wa kitaifa pia ni muhimu kutunza kauli zao, (tungo tata), public figures have to keep their words
 
Watunga Sheria Bungeni nao wanatuangusha! Madhara yake ndio haya.Wanashabikia sana Uchama bila kujali Mambo ya mbeleni
 
Watanzania tuache kulalamika saana tufanye mambo kwa vitendo kama polisi hawawezi kumkamata mafwele kwa nini wananchii tusimdake wenyewe??
 
nakuelewa sana gentleman, kuna mitelezo ya hapa na pale inafahamika πŸ‘Š
Hata mimi nakuelewa, tunaweza wasemea vizuri hawa viongozi wa kitaifa lakini tungo zao tata hutengeza agenda.

Picha ya kibinafsi, (self-image), nitabia ambayo binadamu huihifadhi kwa muda mrefu anaishi nayo kuibadilisha huwa ni ngumu kidogo, mara nyingi hii tabia hutu gharimu, wengine hufanikiwa wengine hupata muelekeo hasi
 
Uwezo huo hana/ hawana. CCM mi genge la wahuni tu,linalolindwa na genge linguine la Police.
 
Kwa hili andiko ndio wanaita uchochezi na taharuki?!!
Wapi ilizuka taharuki?!!
 
Wewe Mneki ungetuelewesha kama ameandika uongo au la maana wewe ndio upo jikoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…