Katibu mkuu wa CCM tunaomba utembelee Kata ya Matundasi iliyopo Wilaya ya Chunya, vijiji vyote Tangu uhuru havijawahi kupata maji safi na salama

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kwa masikitiko makubwa na hizi ni kubwa, ninaomba kumjulisha Katibu Mkuu wa CCM kuwa, Kata ya Matundasi iliyopo Wilaya ya Chunya, mkoa wa mbeya.

Haina maji safi na salama Tangu Tanzania upate uhuru hadi leo.
Kata ya Matundasi ina vitongoji vifuatavyo:-
Itumbi
Kisimani
Makatang'ombe
Matondo
Matundasi a
Matundasi b
Nanyuki
Nzingwa

Vitongoji vyote hivi vinaongozwa na CCM , Diwani wa CCM, Mbunge wa CCM .

Kumekuwa na kuibuka Kwa magonjwa na wananchi wengi hawana vyoo , wanajisaidia porini, hakuna maji safi na salama, hakuna Tarura( barabara ni mbovu) , hakuna shule za msingi na za sekondari za kutosha idadi ya wananchi walioko maeneo hayo, hakuna mitandao ya simu, hakuna vituo vya polisi, hakuna zahanati za kutodha idadi ya watu, ninsomba Katibu mkuu wa CCM atembelee kata hii akiwa na viongozi au mawaziri wafuatao:-

1. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.- Hakuna vituo vya polisi
2. Waziri wa Maji ( Juma Aweso) - Hajuna maji safi na salama
3. Waziri wa Afya- Hakuna vituo vya afya na wananchi wanajisaidua porini.
4. Waziri wa Elimu - Hakuna shule za msingi na sekondari wala chuo.
5. Waziri wa mawasiliano- Hakuna mawasiliano ya simu.
6. Waziri wa ujenzi - Hakuna Barabara za kudumu.
7. Waziri wa Madini - Aje aone wananchi wanavyo zalisha madini na hawapati huduma taja hapi juu.

Tutashukuru iwapo ujio wa kiongozi huyu itafanyika mapema kuinusuru kata ya matundasi na wananchi wake.
 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini Mhandisi Victor H. Seff ametekeleza ahadi ya kuhakikisha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE imetoa mafunzo maalum kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na usawa wa jinsia katika utekelezaji wa mradi wa RISE.

ENDELEA KUSOMA ZAIDI HAPAπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…