Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza amani Tanzania

Uchaguzi 2020 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza amani Tanzania

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Umoja wa Mataifa watoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wafuasi wao kujiepusha na visa vya vurugu nchini Tanzania

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Tanzania kuhakikisha uchaguzi mkuu wa Oktoba 28 unafanyika kwa njia ya amani.

Katika taarifa siku ya Jumatatu iliyotolewa kwa niaba ya Bw. Antonio Gutteres inasema mchakato shirikishi wa uchaguzi na ushiriki mpana wa vyama vya siasa na wagombea wao, haswa wanawake, unabaki muhimu kwa kulinda maendeleo yaliyofanywa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha utulivu, demokrasia na maendeleo endelevu.

Katibu mkuu wa Umoja huo pia ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wafuasi wao kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani na kujiepusha na visa vya vurugu.

Mamlaka pia imetakiwa kutoa mazingira salama ambayo yatawawezesha Watanzania kutekeleza haki yao ya kiraia na kisiasa.

1603826964253.png
 
Wambie wasiwe na wasi wasi juu ya amani yetu. Hakuna Mtanzania ataacha kutafuta riziki yake na familia yake kisa kwenda kumpigania Mwanasiasa mmoja ulaji wake.

Naipongeza pia TCRA kwa kuithibiti mitandao ya kijamii katika nyakati hizi za uchaguzi hii italifanya Taifa letu kuwa salama ndani na nje ya nchi kuhusiana na Mambo ya "ciber intelligence". Hata USA wakati wa uchaguzi huthibiti Internet zao kuepusha Hackers na Mambo Mengine ya kimutandao..

I love my country [emoji1241]
 
Back
Top Bottom