LGE2024 Katibu Mwenezi Ada Tadea Taifa amvaa Lema amtaka aache maneno. Wapinzani tujipange Uchaguzi ujao 2029

LGE2024 Katibu Mwenezi Ada Tadea Taifa amvaa Lema amtaka aache maneno. Wapinzani tujipange Uchaguzi ujao 2029

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
25 October 2024

Zuberi Mwinyi Katibu Mwenezi taifa wa ADA TADEA " Wapinzani Hatukujiandaa kwa Uchaguzi wa TAMISEMI 2024, Tusiilaimu CCM


View: https://m.youtube.com/watch?v=WKMTl38WQd8

Zuberi Mwinyi anaongeza kuwa vyama vya upinzani vyote Tanzania hatuna mawakala, hatuna wanachama wa kukifadhili kama ilivyo kwa CCM.

Bwana Zuberi Mwinyi anaona kuwa CCM imejipanga vizuri kutokana na uwezo wake wa kifedha, huku vyama vya upinzani vimeshinda hata kuwapa posho ya chakula kwa mawakala wake.

Kuhusu CHADEMA kutilia shaka idadi ya waliojiandikisha katika daftari la mkaazi kuwa kubwa kuliko idadi ya watu kama ilivyobainishwa katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kitaifa.

Katibu huyo mwenezi kitaifa wa ADA TADEA anasema huko kuhoji idadi ya watu kupitiliza wingi kuliko Sensa ya 2022 ni kujaribu kutengeneza uchochezi, wapinzani tujipange kwa uchaguzi mwingine wa TAMISEMI 2029 kwa kuwa huu wa 2024 hatujajipanga sisi wapinzani...

TOKA MAKTABA:
Soma :


 
Vyama vidogo vitakuwa vimetumwa kusema sisi wapinzani pamoja na CHADEMA hatujajipanga 2024

TOKA MAKTABA :

17 February 2023


MALALAMIKO YA VYAMA RAFIKI WA CCM DHIDI YA UKUBWA WA CHADEMA

Kelele hizi mara kuunda baraza la vyama vya siasa au kusikia vyama vilivyo chini ya chama dola kongwe vinalalamika kwanini CHADEMA ni maarufu kiasi taifa zima linasikilizia kila kinachoendelea kuhusu chama cha Demokrasia na Maendeleo ya kweli kwa waTanzania wote, ni moja ya mbinu za chama dola kongwe pamoja na vyama vya mfukoni rafiki vya CCM kukatisha matumaini, imani waliyonayo juu ya CHADEMA.

Mzee John Cheyo - Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki



Mwenyekiti wa chama cha UDP Mh. John Cheyo alalamika siasa kuwekwa "gredi" vyama gani vinaweza kujadili katiba ya nchi, maana kwa sasa suala hili linajadiliwa na vyama viwili tu kimoja kinajiita ni tawala na kingine ni chama 'kikubwa' huku vyama vingine vinavyoitwa vya mfukoni vikiachwa nje ya mjadala huu mkubwa.

Mzee Cheyo anasema umri wake umamueleza kuwa leo chama kinaweza kuwa kikubwa na tawala lakini kesho kikawa kidogo hivyo ikitokea mazungumzo muhimu je chama hicho huko miaka ijayo kitabaguliwa ?
 
26 October 2024
Tarime, Mara
Tanzania

TARIME HALI MBAYA KWA CCM, BAADHI YA MITAA WAMESHINDWA KUTEUA WAGOMBEA

View: https://m.youtube.com/watch?v=PEOQamQJHF4
Kada mkongwe wa CCM asimulia hali ilivyo ngumu kisiasa Tarime mjini, matumaini ya kuishinda CHADEMA katika uchaguzi wa serikali za mitaa ni finyu... sababu minyukano ya ndani ya chama dola kongwe na uimara wa mtandao wa CHADEMA mkoani Mara Tanzania

CCM yashindwa kupata wanaowania nafasi za uongozi wa mitaa, CHADEMA imetamalaki kila kona .... asema kada mkongwe anayeshiriki shughuli za chama dola kwa miaka 45 tangu mwaka 1979 ..
 
Siku zote ADA TADEA huwa hawajajitayarisha na kulaumu wapinzani

TOKA MAKTABA:

October 2020


View: https://m.youtube.com/watch?v=NLsd21vLzq8
Mwanasiasa mkongwe John Magile Shibuda ambaye pia ni mgombea urais kupitia chama cha ADA TADEA, amefanya mahojiano na mtangazaji Charles William, ambapo pamoja na mambo mengine ameeleza sababu zinazofanya asionekane akifanya mikutano mingi ya hadhara ya kampeni za urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania......

1729944660867.jpeg


ADA TADEA WATU WA BRIEF CASE / MIKOBA KUSUBIRI FURSA

1729944781066.jpeg

2020 mgombea wa ADA TADEA mheshimiwa John Shibuda, mgombea wa chama rafiki wa CCM
 

Ada-Tadea yataka Tume huru kabla ya 2025​

Jumatano, Mei 25, 2022
1729945334323.jpeg

Mwenyekiti Chama cha Ada-Tadea, John Shibuda

By Kelvin Matandiko mwandishi wa habari wa Mwananchi

Muktasari:​

Chama cha Ada-Tadea kimeshauri upatikanaji wa Tume huru ya Uchaguzi kabla uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na ule mkuu 2025.

Dar es Salaam. Chama cha Ada-Tadea kimeshauri upatikanaji wa Tume huru ya Uchaguzi kabla uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na ule mkuu 2025.

Chama hicho ni miongoni mwa vyama vinne vinavyotoa maoni yake mbele kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia nchini.

Vyama vingine ni UPDP, AFP na ADC. Akizungumza leo Jumatano Mei 25, 2022 baada ya kuwasilisha maoni, Mwenyekiti wa chama hicho, John Shibuda amesema chama hicho kimewasilisha mapendekezo katika maeneo yote tisa ikiwamo suala la tume hiyo inayohitajika mapema.

“Tume itazamwe upya teuzi zake, kuwepo na maboresho yatakayojenga imani kwa wananchi na wadau wa siasa, ambao wataona kwamba tume hii sasa inakuwa wasimamizi wanaotekeleza majukumu yao kwa uhuru,” amesema.​


“Kwa sababu maandalizi ya tume huru haihitaji pesa nyingi kama masuala ya Katiba, basi ni muhimu marekebisho haya yafanyike haraka iwezekanavyo kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa na ule uchaguzi mkuu 2025.”

Kuhusu hoja ya katiba, mwenyekiti huyo wa zamani wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini amesema ni muhimu kufanyia marekebisho ya andiko jipya la katiba badala ya kuendelea na katiba pendekezwa au iliyopo sasa.
 
25 October 2024

Zuberi Mwinyi Katibu Mwenezi taifa wa ADA TADEA " Wapinzani Hatukujiandaa kwa Uchaguzi wa TAMISEMI 2024, Tusiilaimu CCM


View: https://m.youtube.com/watch?v=WKMTl38WQd8

Zuberi Mwinyi anaongeza kuwa vyama vya upinzani vyote Tanzania hatuna mawakala, hatuna wanachama wa kukifadhili kama ilivyo kwa CCM.

Bwana Zuberi Mwinyi anaona kuwa CCM imejipanga vizuri kutokana na uwezo wake wa kifedha, huku vyama vya upinzani vimeshinda hata kuwapa posho ya chakula kwa mawakala wake.

Kuhusu CHADEMA kutilia shaka idadi ya waliojiandikisha katika daftari la mkaazi kuwa kubwa kuliko idadi ya watu kama ilivyobainishwa katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kitaifa.

Katibu huyo mwenezi kitaifa wa ADA TADEA anasema huko kuhoji idadi ya watu kupitiliza wingi kuliko Sensa ya 2022 ni kujaribu kutengeneza uchochezi, wapinzani tujipange kwa uchaguzi mwingine wa TAMISEMI 2029 kwa kuwa huu wa 2024 hatujajipanga sisi wapinzani...

TOKA MAKTABA:

Wao hawa ADA TADEA hawawezi kujiongelea wao, bali wao huwa wanasubiri tu cdm waongee halafu watumwe kwenda kukanusha wanachosema cdm?!
 
Vyama rafiki vya CCM vimetumwa kusambaza propaganda dhidi ya CHADEMA tishio kwa chama dola kongwe.
 
Jamaa anaamini kabisa yupo kwenye kundi la wapinzani ?

1000012512.jpg
 
Songea, Ruvuma

MAMBO MOTO CHADEMA KANDA YA KUSINI, HATUKIMBII UCHAGUZI WA TAMISEMI 2024 CCM WEPESI


View: https://m.youtube.com/watch?v=6TNTBai-_RU

Mwenyekiti wa CHADEMA kanda mpya ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi kamanda Aden Mayala aongea mazito ...

Chama kongwe kimechoka ndiyo maana CHADEMA sasa hivi haina mpinzani katika vyama vya siasa viliiyoandikishwa, ndiyo maana CCM inatanguliza vyombo vya dola kupambana na CHADEMA

Mbali na hilo kiongozi wa ngazi ya kata CHADEMA walivyo vizuri anaweza kupambana na kiongozi wa CCM wilaya ndiyo maana hata uchaguzi huu wa TAMISEMI unasimamiwa na viongozi wa serikali walio makada wa CCM

Hata hivyo 2024 CHADEMA hatujakimbia tutapambana kisiasa na CCM pamoja na vyama rafiki wa CCM na makada wa CCM waliopo serikalini...
 
CHADEMA WAKABILIANA NA PROGAGANDA ZA MBUNGE MRISHO GAMBO


View: https://m.youtube.com/watch?v=otIk27rFtRU

Mrisho Gambo hawezi kuwa msemaji wa CHADEMA kanda ya Kaskazini, .... CHADEMA ipo imara haihitaji msemaji aliye nje ya chama kama kada mbunge wa CCM Mrisho Gambo ...

Mrisho Gambo hawezi kuionea huruma taasisi ya chama kikubwa kama CHADEMA kwa kutimia propaganda zisizo na ukweli .... CHADEMA kanda ya kaskazini yamueleza mbunge huyo wa CCM Mrisho Gambo ..
 
Rungwè, Mbeya
Tanzania

VIONGOZI WA CHADEMA WAENDELEA KUWEZESHWA KWA MAFUNZO


View: https://m.youtube.com/watch?v=_2YCljrfDB0

Mkufunzi wa CHADEMA kamanda Emily Mwakilembe aendelea kuwawezesha wanachama kwa semina za mafunzo elekezi kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Uchaguzi za Serikali za Mitaa utakaohitimishwa tarehe 27 November 2024 kwa kura kupigwa nchi nzima .
 
Membe, Chamwino
Dodoma

KIJIJI CHA MEMBE CHAMWINO DODOMA, KIONGOZI ATIMKIA CHADEMA

View: https://m.youtube.com/watch?v=XReNaqCbXoQ

Kiongozi huyo wa CCM kijiji cha Membe Chamwino atimka na kukiacha chama dola kongwe, na kuongea mazito juu ya mfumo wa kiuongozi wa chama dola kabla ya kukaribishwa kujiunga na CHADEMA mbele ya mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Dodoma kamanda Aisha Madoga ...

Kiongozi huyo wa kijiji cha Membe tarafa ya Membe Chamwino Dodoma kwa kina hali ya dhahma, vurugu na kukosekana haki inayoendelea kutokana na uroho wa madaraka ndani ya CCM bila kujali maendeleo ya watu
 
28 October 2024
WASALITI NDANI YA CCM WANABEBWA NA MTEMVU
1730115505960.jpeg

Picha maktaba : Abbas Mtemvu Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam

HABARI ZAIDI, CCM TEMEKE WAANDAMANA KUPINGA UCHAGUZI WA NDANI KUVURUGWA

"HATUTASHIRIKI UCHAGUZI" CCM HAPATOSHI, WAGOMBEA WAGOMEA MAAMUZI YA CHAMA WASEMA **** HUJUMA

Wanachama kata ya Nzasa Temeke jijini Dar es Salaam waongea mazito,....

View: https://m.youtube.com/watch?v=Xtiju5onaa8

Kata za mitaa ya Madale, Nzasa, Tandika Maguruwe n.k jijini Dar es Salaam uchaguzi wa ndani kuvurugwa wamtuhumu mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Mtemvu kwa kikivuruga chama kongwe dola, na kwa hali hiyo viongozi wa matawi wilaya ya Temeke Tandika waingia hofu wapinzani kupita bila kupingwa katika uchaguzi baada ya chama dola kongwe kukumbwa na wimbi la mvurugano ktk mchakato wa uchaguzi wa ndani ya CCM...
 
Back
Top Bottom