PreGE2025 Katibu Uenezi CCM Amos Makalla: CHADEMA wanapumzika wamechoka huu mwendo hawauwezi na sisi tumewakubalia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema wamewakubalia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupumzika.

Aliyasema hayo April 13 wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa Lionja, Kata Lionja, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, waliofika kumpokea kwa ajili ya mwendelezo wa ziada yake ya siku 10 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

makalla.png

“Na uzuri niseme nisiseme, wanapumzika wamechoka huu mwendo hawauwezi na sisi tumewakubalia," amesema.

Makalla amewapa pole wananchi kwa matusi na kejeli na kuwaeleza wamekuja wao wenye dhamana nao kuwaelezea miradi iliyotekelezwa na serikali.

Soma pia: Amos Makalla: Umma hauandaliwi kwa nguvu, unakubali wenyewe

Kadhalika amewaeleza namna nchi inavyoelekea kwenye maendeleo, huku akiwasisitizia kwamba, amani na utulivu imeasisiwa na Chama Cha Mapinduzi.

Source: Nipashe
 
Boya huwa jepesi kweli kwenye maji, linaelea tu bila direction maalumu.
 
CHADEMA wanapumzika au wako kuagiza virus vya Ebola na epoxy?.
 
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema wamewakubalia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupumzika.

Aliyasema hayo April 13 wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa Lionja, Kata Lionja, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, waliofika kumpokea kwa ajili ya mwendelezo wa ziada yake ya siku 10 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

“Na uzuri niseme nisiseme, wanapumzika wamechoka huu mwendo hawauwezi na sisi tumewakubalia," amesema.

Makalla amewapa pole wananchi kwa matusi na kejeli na kuwaeleza wamekuja wao wenye dhamana nao kuwaelezea miradi iliyotekelezwa na serikali.

Soma pia: Amos Makalla: Umma hauandaliwi kwa nguvu, unakubali wenyewe

Kadhalika amewaeleza namna nchi inavyoelekea kwenye maendeleo, huku akiwasisitizia kwamba, amani na utulivu imeasisiwa na Chama Cha Mapinduzi.

Source: Nipashe

Kauli ya Amos Makalla kwamba “CHADEMA wamechoka na tumewakubalia kupumzika” ni jaribio dhaifu la kuchekesha hadhira iliyochoka kwa propaganda. Hii si hoja ya kisiasa, ni kejeli ya mtu anayetegemea kelele kufunika ukimya wa hofu ndani ya mfumo unaoyumba.

Makalla amepotosha kwa makusudi — CHADEMA haijachoka, bali imechoka kushiriki michezo michafu ya uchaguzi isiyo na tume huru, isiyo na haki, na isiyo na uhalali wa kidemokrasia. Hicho ndicho kipumziko anachozungumzia. Ni mapumziko ya heshima, si dalili ya kushindwa.

Kwa kutumia lugha ya kisiasa: ni kama askari kukataa kuingia vitani akiwa hana silaha wala ulinzi, kisha adui akaanza kumkejeli kwamba ameogopa mapigano. Huo si ushindi wa adui, ni ujinga wa kufikiri vita ni ujasiri wa kujiua bila sababu.

Makalla anasema CHADEMA imechoka na haimudu mwendo — lakini hajatuambia ni mwendo gani? Mwendo wa kukandamiza vyama? Kuzuia mikutano? Kueneza miradi hewa? Au mwendo wa propaganda zisizovutia tena hata mashabiki wa CCM? Kama huo ndiyo mwendo, basi si CHADEMA tu, bali taifa zima limechoka.

Na kuhusu "amani na utulivu kuasisiwa na CCM" — hiyo ni kauli inayodharau historia ya Watanzania. Amani ya kweli hujengwa na haki, usawa, na taasisi imara — siyo kwa mikutano ya chama kimoja wala kwa kauli za majukwaani. Kama CCM ingeasisi amani ya kweli, isingeendelea kutumia polisi na dola kukandamiza wapinzani.

Makalla anapaswa kujua kwamba kuna tofauti kati ya "kupumzika kwa mpito" na "kusalimu amri". CHADEMA haijasalimu amri — inajiweka sawa kwa mapambano ya kidemokrasia kwa viwango vya juu zaidi.

Na historia inatufundisha hivi:
➡ Vyama vya mabadiliko havifi — huchukua pumzi.
➡ Mifumo ya mabavu huonekana imara — mpaka siku yanapoanguka kwa kishindo.
➡ Na kejeli za watawala huwa nyimbo za mwisho kabla ya kizazi kipya kusimama.

Kwa hiyo CPA Makalla, tusiwajibu kwa kelele bali kwa kazi — mabadiliko hayaandaliwi kwa kelele, bali kwa nidhamu ya kimapambano. CHADEMA haijachoka — inajipanga. Na safari hii, haitarudi nyuma.
Wekeni mazingira sawa ya ushindani halafu baada ya uchaguzi muje kutoa kauli kama hizi.
 
KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla, amesema wamewakubalia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupumzika.

Aliyasema hayo April 13 wakati akizungumza na wananchi wa Tarafa Lionja, Kata Lionja, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, waliofika kumpokea kwa ajili ya mwendelezo wa ziada yake ya siku 10 katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

“Na uzuri niseme nisiseme, wanapumzika wamechoka huu mwendo hawauwezi na sisi tumewakubalia," amesema.

Makalla amewapa pole wananchi kwa matusi na kejeli na kuwaeleza wamekuja wao wenye dhamana nao kuwaelezea miradi iliyotekelezwa na serikali.

Soma pia: Amos Makalla: Umma hauandaliwi kwa nguvu, unakubali wenyewe

Kadhalika amewaeleza namna nchi inavyoelekea kwenye maendeleo, huku akiwasisitizia kwamba, amani na utulivu imeasisiwa na Chama Cha Mapinduzi.

Source: Nipashe
 
Attachments

  • cf0ea736521de32f5d65e1a6b7fd56a4_1743187151179.mp4
    579.6 KB
Back
Top Bottom