Baada ya Mwenyekiti, Katibu wa Jumuiya wa Walimu Wasio Na Ajira (NETO) naye adaiwa kukamatwa na Jeshi La Polisi usiku huu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Baada ya jana kukamatwa kwa Mwenyekiti wa NETO, leo zimeibuka taarifa kwamba Katibu wa Jumuiua hiyo amekamtwa na Jeshi La Polisi.

Kupitia mtandao wa X, NETO waliandika kwamba:

Katibu NETO Bw. Daniel Edger Mkinga amekamatiwa Kibaha Miembe Saba nyumbani kwake majira ya usiku wa saa tatu kasoro. Waliofika nyumbani kwake kumkamata ni Balozi, Mjumbe na Askari 3 kutoka kituo cha Polisi Maili Moja Kibaha, Pwani.

katibu neto.png

Taarifa zinadai kwamba Bw. Daniel Edger Mkinga amekamatwa nyumbani kwake, Kibaha Miembe Saba, majira ya usiku wa saa tatu kasoro. Waliotekeleza ukamataji huo ni Balozi wa mtaa, Mjumbe na askari watatu kutoka Kituo cha Polisi Maili Moja, Kibaha, Pwani.

kisabo .png

netoo.png
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), Daniel Edigar Mkinga, amedaiwa kukamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani akiwa nyumbani kwake Kibaha, Miembe Saba majira ya saa tatu kasoro usiku wa siku ya Jumanne Februari 25, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa alizotoa mke wake, Mkinga alikamatwa na askari watatu kutoka kituo cha Polisi Maili Moja Kibaha, katika ushuhuda wa viongozi wa mtaa wake akiwemo Balozi na Mjumbe.

Screenshot 2025-02-26 091302.png
Taarifa iliyotolewa na NETO tarehe 25 Februari 2025, inaeleza kuwa Mkinga anashikiliwa kwa tuhuma zinazohusiana na ushiriki wake katika jumuiya hiyo. Agness Mpundi, Makamu Mwenyekiti wa NETO, ametoa wito kwa wanasheria na mashirika ya haki za binadamu kusaidia kuhakikisha Mkinga anapata uhuru wake.

"Tunaendelea kuwakumbusha kuwa NETO si chama cha siasa, wala haina nia yoyote ovu dhidi ya amani ya nchi yetu. Umoja huu unahimiza serikali kutoa ajira kwa walimu na kutekeleza makala tulizoandika kwa mamlaka husika," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo, huku NETO ikisisitiza kuwa itaendelea kupigania haki ya walimu wasio na ajira na kuomba serikali ifanyie kazi madai yao.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umelaani vikali kukamatwa kwa Mkinga ikieleza kuwa imechukua hatua za kisheria kwa kumtuma wakili wake kufuatilia dhamana ya Mkinga na imelitaka Jeshi la Polisi kumuachia mara moja, kwani hakuna kosa lolote alilotenda kwa kudai haki za walimu, hata hivyo juhudi za kupata kauli ya polisi juu ya kukamatwa kwa Mkinga bado zinaendelea.

"Hatutaacha kufuatilia suala hili kuhakikisha kuwa Katibu wa NETO anapata haki zake kwa mujibu wa sheria," imeeleza THRDC katika tamko lake rasmi.

Madai ya kukamatwa kwa Katibu Mkuu NETO yanakuja saaa chache baada ya Jeshi la Polisi mkoa wa Geita kukiri kumshikilia Joseph Paul (31), Mwenyekiti wa NETO kwa ajili ya mahojiano kutokana na madai ya kuhusika na kundi hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita SACP Safia Jongo, Paul alikamatwa Februari 24, 2025, baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa umoja huo hauna usajili rasmi kutoka kwa mamlaka husika.

Polisi walisema mtuhumiwa alihojiwa kwa mujibu wa sheria, kuelezwa tuhuma dhidi yake, na kwa sasa yuko nje kwa dhamana

Soma, Pia
 
Walilitafuta wamelipata, kwa serikali za Africa ni waoga sana kwa vuguvugu yoyote.
 
Haka ka mchezo kanaanza ki masihara masihara lakini kwa sie ma time traveler, naona hii ishu ni threat, serekali liangalieni hili vizuri.

Hii ishu ikifikia stage ya pili na tatizo ndio litalipukia hapo, huo moto ukiwaka ni ngumu sana kuuzima, na hapo ndio mtandao wa X utakapoanza mambo yake.

Baada ya hapo ni stage no 3

Serekali inatakiwa Icheze vizuri sana na hii kete, hii kete ni ya moto,akicheza vibaya, kuna watu wanaingia kingi, na hapo ndio patakua pabaya.

Sio kwamba nafurahia au nashauri serekani ikamate watu, ila sijui ita deal vipi na hili tatizo
 
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita SACP Safia Jongo, Paul alikamatwa Februari 24, 2025, baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa umoja huo hauna usajili rasmi kutoka kwa mamlaka husika.Ni

Polisi walisema mtuhumiwa alihojiwa kwa mujibu wa sheria, kuelezwa tuhuma dhidi yake, na kwa sasa yuko nje kwa dhamana

Soma, Pia
Ni Rasmi tuko kwenye pori la wanyama wakali kila mmoja ajihami!!
 
Serikali kuboresha maslahi ya watumishi, kutoa ajira na kutatua changamoto haitaki ila inatumia nguvu nyingi kuwaumiza hao hao inaowanyima haki zao.

Kuna namna nchi za Kiafrica haziko sawa.
 
Bado wapuuzi hao wanaendelea kukamatwa? Bado mweka hazina wao, hawa vijana huwa wanajiona wajuaji sana wanapokuwa vyuoni wanadhani mazingira ya kusoma chuoni na sawa na kuwa kazini. Wanashinikiza waajiriwe kana kwamba serikali ina nafasi nyingi za kuwaajiri za kuwaajiri kwa pamoja. Wengine hawataajiriwa mpaka watazeekea mitaani, ni bora wajiongeze kufanya shughuli zingine waache uvivu wa kuthubutu kuanzisha shughuli zao. Wana mentality mbovu kudhani ukisomea fani fulani ni lazima uajiriwe kwayo
 
Haka ka mchezo kanaanza ki masihara masihara lakini kwa sie ma time traveler, naona hii ishu ni threat, serekali liangalieni hili vizuri.

Hii ishu ikifikia stage ya pili na tatizo ndio litalipukia hapo, huo moto ukiwaka ni ngumu sana kuuzima, na hapo ndio mtandao wa X utakapoanza mambo yake.

Baada ya hapo ni stage no 3

Serekali inatakiwa Icheze vizuri sana na hii kete, hii kete ni ya moto,akicheza vibaya, kuna watu wanaingia kingi, na hapo ndio patakua pabaya.

Sio kwamba nafurahia au nashauri serekani ikamate watu, ila sijui ita deal vipi na hili tatizo
Hakuna wa kuiweza serikali wewe... Hao wote wanacheza tu. Serikali ina mikono nj miguu mirefu mno
 
Back
Top Bottom