KATIBU wa CCM Iringa afutwa kazi kwa tuhuma za ulevi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
KATIBU wa CCM Mkoa wa Iringa, Said Goha, amefutwa kazi na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, kwa tuhuma za ulevi uliokithiri unaodaiwa kuchafua taswira ya chama hicho tawala.

Chacha ametoa uamuzi huo wakati akizungumza katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa, uliohusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa CCM na Jumuiya zake mwaka 2027, pamoja na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya chama hicho.

Amesema Goha atapangiwa majukumu mengine ndani ya chama, huku CCM ikimtafuta atakayechukua nafasi yake, kwa kipindi hiki, amesema chama kitaendelea kuongozwa na Katibu mwingine hadi atakapopatikana atakayeziba nafasi hiyo.

Chacha amesisitiza kuwa CCM haitamfumbia macho kiongozi au mwanachama ambaye mwenendo wake unakiweka chama katika taswira isiyofaa, akisisitiza umuhimu wa nidhamu na kulinda heshima ya chama.

Your browser is not able to display this video.
 
Je,huwa anaingia ofisini,vikaoni au mikutanoni amelewa?Ameharibu kazi zake za ukatibu?Huwa analewa wakati wa kazi?Kuna hasara aliyowaletea hao CCM?Mmeshaanza kuchawiana.
 
Wapo wengi tuu walevi.
Wamama wanagawa balaa.
Vijana full uchawa na umalaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…