PreGE2025 Katibu wa CCM Iringa awataka Viongozi kudumisha Umoja na Mshikamano kuelekea Uchaguzi

PreGE2025 Katibu wa CCM Iringa awataka Viongozi kudumisha Umoja na Mshikamano kuelekea Uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
418
Reaction score
550
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Saidi Goha, akiambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM mkoa, ameendesha semina kwa viongozi wa chama na jumuiya zake kuanzia ngazi ya matawi na kata katika Wilaya ya Iringa Vijijini.

Katika mkutano huo, Goha alieleza kufurahishwa na mshikamano mzuri uliopo ndani ya chama katika wilaya hiyo na kuwasihi viongozi kuendelea kudumisha umoja na upendo, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza na viongozi wa matawi na kata katika kata nne za Iringa Vijijini, Katibu wa CCM aliwataka viongozi hao kujiepusha na makundi ya kisiasa kwa sasa, akisisitiza kuwa viongozi waliopo bado wapo madarakani.

Amesisitiza umuhimu wa utulivu na mshikamano ndani ya chama kwa ajili ya ustawi wa CCM na maendeleo ya wananchi.

"Wilaya yenu imetulia, hivyo nawaomba viongozi twendeni tukafanye ziara mbalimbali za kazi ili kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Ni muhimu kueleza wananchi kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameleta miradi mikubwa ya kimkakati katika kata zenu," alisema Goha.

Goha aliwataka viongozi wa CCM katika ngazi zote kuwa mstari wa mbele katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitendo, akisisitiza kuwa chama hakiwezi kuwa imara bila viongozi waadilifu na wenye kushikamana. Alisema mshikamano wa viongozi ni silaha muhimu ya ushindi kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo akawataka kuepuka migawanyiko na badala yake kuendelea kushirikiana kwa lengo la kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo.

Alisisitiza kuwa ushindi wa CCM hauji kwa bahati, bali kwa kazi na ushirikiano wa dhati kutoka kwa viongozi na wanachama wote wa chama hicho tawala. Aliwataka viongozi kuhakikisha wanawafikia wananchi, kueleza mafanikio ya chama na kuhamasisha mshikamano kwa ajili ya ushindi wa CCM katika uchaguzi ujao.

Snapinsta.app_480964556_1153857250104975_3767432666814955864_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom