Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Mlali Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Herieth Ngonde amedai kushambuliwa na Diwani wa kata hiyo aliyetambulika kwa Frank Mwananziche kwa kupigwa wakati wa kikao cha siasa kilichokuwa kinajadili maendeleo ya chama hicho
Akizungumza na wanahabari katibu wa chama hicho amesema diwani huyo amemshambulia mara baada ya kutofautiana kauli katika kikao hicho
Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo anayedaiwa kufanya tukio hilo amesema kuwa kwa sasa suala hilo lipo chini ya chama cha Mapinduzi,na mpaka sasa jitihada za kulisaka jeshi la polisi zinaendelea kwaajili ya ufafanuzi zaidi.