Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Iringa Mjini, Pascal Chibala amehamia na kutangazwa rasmi kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Chibala ameeleza kuwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi unaofanywa na CCM ni sababu kubwa ya kumfanya ahamie chama hicho kwani kinajitanabaisha kwa kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za wananchi wake.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Chibala amehamia rasmi na kutangazwa kuwa mwanachama mpya wa CCM leo Machi 29,2024 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mwembetogwa ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafuzo wa CCM, Amos Makalla katika mikoa ya Mbeya na Iringa.
Baada ya Chibala kutangazwa kuwa mwanachama mpya wa CCM,Makalla alitoa maagizo kwa uongozi wa chama hicho Iringa kumpa usajili rasmi Chibala ili aweze kuwa mwanachama aliyekamilika.