PreGE2025 Katibu wa CHADEMA kanda ya ziwa awataka viongozi wa dini kutoyumbishwa na wanasiasa

PreGE2025 Katibu wa CHADEMA kanda ya ziwa awataka viongozi wa dini kutoyumbishwa na wanasiasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Zakaria Obadi amekosoa kitendo cha baadhi ya wanasiasa kukosoa viongozi wa dini kujihusisha na siasa kuwa huo ni uoga.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amewataka viongozi wa dini kutokuyumbishwa na maneno hayo huku akisisitiza kuendelea kuzungumza ukweli na kukemea vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

"Ni waombe viongozi wa dini wasiyumbishwe na wanasiasa wanaotaka kujibanza kwenye mgongo wa siasa, wasirudi nyuma, hii habari ya kwamba viongozi wa dini wasijihusishe na siasa huo ni uoga tu ni hofu ambayo wanaitengeneza ili ukweli usizungumzwe," amesema.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha Obadi mbali na kutoa pole kwa viongozi na waumini wa dini ya Kikatoriki kufuatia tukio la kushambuliwa kwa katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Dkt. Charles Kitima amezitaka taasisi za dini kuungana kupinga vitendo hivyo

"Nitumie nafasi hii kumpa pole Padri Kitima pamoja na kanisa la Katoliki nchini kwa kitendo cha kushambuliwa kwa kiongozi wao ambaye hana hatia yeyote na amekuwa akisimama kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Tanzania akisimama kwenye misingi ya kusema ukweli, haki, kutetea uhuru na kuhamasisha jamii iwe na tabia ya kuelewa mambo," amesema.
 
Back
Top Bottom