LGE2024 Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Singida achomwa Kisu na kijana wa CCM akiwa eneo la kupiga kura

LGE2024 Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Singida achomwa Kisu na kijana wa CCM akiwa eneo la kupiga kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Singida Mjini, Hamis Nkua, amechomwa kisu katika mkono wa kushoto begani.

Akizungumza na Nipashe Digital katika Hospitali ya Rufaa ya Mandewa ya Mkoa wa Singida ,amesema amechomwa kisu leo Novemba 27, 2024 saa 8:00 mchana katika eneo la Unyankae kata ya Mandewa Manispaa ya Singida.

Nkua ambaye wakati akizungumza nguo zake zilikuwa zimetapakaa damu,amesema amechomwa kisu wakati alipokwenda na Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya Singida mjini,Swahiba Mwanga eneo ka Unyankae baada ya kupigiwa simu na viongozi wa kata wa chama hicho kwamba wamevamiwa.
Aliyekinyuma na Haki Makazi Yake Jehanamu
Asalam Aleykum
 
Haya mauaji yanayoendelea kwa wana chama, viongozi na wwgombea wa nafasi mbalimbali kwenye huu uchafuzi wa serikali za mitaa ni kielelezo tosha kabisa kwamba CCM imekwisha kabisa

Walianza kuteka, kutesa, kujeruhi, kupoteza na kuua wapinzani wao kisiasa hasa CHADEMA lakini sasa wanafanya waziwazi bila kificho
Ni hofu gani hii kubwa kabisa iliyowakumba mpaka wanafanya mauaji mengi kiasi hiki
Wataua wangapi!
Watajeruhi eangapi!
Watapoteza wangapi!
Kila wanachofanya kwasasa wanazidi kuharibu

Ogopa sana mateke ya mwisho ya ng'ombe aliyekata roho..hii ndio ccm ilipofikia kwasasa
Uchaguzi tu wa serikali za mitaa watu wanamwaga damu?

Eeh Baba Mungu tutazame kwa jicho la Huruma
 
Back
Top Bottom