Katibu wa Itikadi CCM, Shaka kwa Wasira: Nitaendelea kujifunza ili niwe bora zaidi

Katibu wa Itikadi CCM, Shaka kwa Wasira: Nitaendelea kujifunza ili niwe bora zaidi

Naona mzee anajaribu kutengeneza njia ya 2025.
Make mkakati wake sasa anamwandaa mwanae kuja kugombea jimbo la BUNDA MJINI 2025.
Juzi kati ametoka kupambana kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM wilaya ya BUNDA amefanya figisu yeye na Charles KAJEGE wakampitisha SOSPETER MASAMBU GOMBOROJO kuwa mwenyekiti CCM wilaya ya BUNDA kwenye uchaguzi Mdogo.

Naona mzee anapambana mapema kutafuta huruma ya chama kwa mwanae.
Anafanya figisu mnamchekea tu huyo gorilla wakati mahindi bado mabichi shambani, ngoja muone!
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka leo 25 Mei 2021 ametembelewa na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya Taifa Ndg. Steven Masato Wasira katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar Es Salaam.

Katika mazungumzo yao Ndg. Wasira ameeleza na kumumwagia sifa lukuki Ndg. Shaka kwa kazi alizozifanya vyema katika kipindi cha nyuma na kueleza wazi kuwa hawana hofu naye katika nafasi anayoitumikia kwa sasa.

Ndg. Wasira amesema, "Umefanya kazi nzuri sana ukiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar na baadae Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa. Ulichapakazi ya kijasiri, ukijibu mapigo ya upinzani kwa wakati na kwa nguvu ya hoja. Umekuwa ukipangua hoja kwa mirejesho ya kisiasa, kihistoria aidha ya TANU au ya ASP endelea hatuna hofu nawe kwenye nafasi hii."

Ndg. Shaka ameahidi kuwa hatawaangusha na ataendelea kujifunza mambo mbalimbali.
Ndg. Shaka amesema "Siku zote wanasiasa mahiri na mashuhuri sana duniani wamejifunza, kuelekezwa, kuandaliwa, kukoselewa na kushauriwa lakini hatimaye hufahamu na kuwa mweledi hasa ukikubali kujifunza toka kwa wanasiasa waliokutangulia kwani hata walimu nao wana wakufunzi wao, kwa uwezo MwenyeziMungu sitawaangusha."

Kazi Inaendelea, Tufanye kazi kwa maendeleo yetu binafsi na taifa.

View attachment 1797437View attachment 1797439
Kati ya hao wawili ni nani aliyeomba kukutana na mwenzake ?
 
Ukiachana na Siasa Wasira hakuna kingine anakijua...Wasira ni siasa siasa ni Wasira.!

Kuna wakati alifungiwa kugomubea akajaribu kuuza samaki ; akala mtaji hivyo akashindwa kurudisha mkopo wa benki!!! Mzee alichacha mbaya, swahiba wake mkwere akaja kumuokoa!!! Ndio maana mkwere anamtumia sana kupambana na mahasimu zake wa kutoka mikoa ya kanda ya ziwa!!!
 
Wewe ni nyumbu kweri kweri wa Ufipa usiyejua kitu. Hujui kuwa Wassira ni Team Msoga wa kutupwa? Kumnasibisha na JPM ni kuonesha kiwango kikubwa cha ujinga wako.
Dakika ya 80, Team Msoga 4-Team Mwendazake 0
 
Wassira anatafuta nini bado ? Anataka azikwe kitaifa ? Akiwa madarakani? Too much anamtafuta Mama....kwa njia yeyote ile
 
Back
Top Bottom