GE2025 Katibu wa Madereva Bodaboda: Sisi tuna amani chini ya uongozi wa Dkt. Samia, ndiyo maana mambo yanaenda

GE2025 Katibu wa Madereva Bodaboda: Sisi tuna amani chini ya uongozi wa Dkt. Samia, ndiyo maana mambo yanaenda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Katibu wa Umoja wa Madereva Bodaboda Manyoni atoa tamko la kutunza Amani na Ushiriki Uchaguzi Mkuu 2025

Katibu wa Umoja wa Madereva Bodaboda (Maafisa Usafirishaji) Wilaya ya Manyoni, Edward, amesisitiza kuwa madereva wa pikipiki wilayani humo wamejipanga kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika kwa amani na utulivu. Aidha, amebainisha kuwa madereva hao watajitokeza kwa wingi kushiriki katika kupiga kura ili kuchagua viongozi wanaofaa kuiongoza nchi.

Edward aliyasema hayo wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Taifa, Ndg. Geofrey Kiliba, alipokutana na madereva bodaboda wilayani Manyoni kwa lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii katika uchaguzi na kuimarisha mshikamano wa amani.

Aliongeza kuwa madereva bodaboda ni sehemu kubwa ya nguvu kazi ya vijana nchini, hivyo mchango wao katika kulinda amani na kushiriki uchaguzi ni muhimu kwa mustakabali wa taifa.

 
Bodaboda kwenye ubora wao, anasema waheshimiwa wasafirishaji asee
 
Ma Afisa usafirishaji ktk 1 na 2. Na huyo Kiliba aliye disco pale DIT.
😂😂😂😂😂 lol
 
Acha waendelee kutumika huku wanaowatuma wakijinufaisha kwa ufisadi wa kodi zao
 
Back
Top Bottom