PreGE2025 Katibu wa NEC Zanzibar: Serikali zetu hazitohofia kukopa kutekeleza Miradi ya Maendeleo

PreGE2025 Katibu wa NEC Zanzibar: Serikali zetu hazitohofia kukopa kutekeleza Miradi ya Maendeleo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema Serikali zake hazitohofia wala kuacha kukopa kwenye Taasisi za Kimataifa za Fedha na Benki ya Dunia kwa minajili ya kutekeleza shughuli za miradi na ujenzi wa miundombinu .

1743504353617.png
Pia chama hicho kimeahidi kitasimamia ahadi na sera za msingi kwa kumaliza changamoto zote zinazowatatiza wananchi mijini na Vijijini .

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis, ameeeleza hayo mara baada ya kumalizika Baraza la Edd el Fitry lililofanyika kwenye viwanja vya Polisi Ziwani Kisiwani Unguja.

Soma, Pia: Rais Samia: Asiyejua anasema Serikali inakopa tu, kwani tunakopa kununua sare za harusi?

Mbeto alisema serikali za CCM ili ziweze kutekeleza ahadi na ilani yake ya uchaguzi kwa ufasaha ,itafanya kila linalowezekana kwa nia ya kuwaletea wananchi wake maendeleo bila kuogopa kukopa .

Alisema Serikali za CCM hazitacha kutekeleza wajibu wake wa kutumikia wananchi , kumaliza changamoto za kisekta ikiwemo kuimarisha miradi ya Elimu, Afya , Kilimo, Ufugaji , Uvuvi na kupeleka Maji safi na Salama Vijijini.

Ripoti ya CAG: Deni la Serikali lafikia TSh. Trilioni 97.35, ongezeko la TSh. Trilioni 15.1
 
Shibe mbaya sana. Wakati mwingine huleta upofu kumbe.
 
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar Idara ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis,
Unategemea kusikia nn kutoka kwa mvaa makubazi mzanzibari tena anaitwa Khamis!!!???
 
Yeye Yuko sahihi kusema Hivyo Kwa sababu Tanganyika ikiopa mkopo na Zanzibar inapewa asilimia 21 ya huo mkopo lakini atakayelipa Hilo deni ni Tanganyika.
 
Back
Top Bottom