The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amesema walimu ndio kada ya watumishi wa umma wanaolipwa mishahara mikubwa kuliko kada nyingine yoyote.
Naibu Katibu Mkuu amesisitiza kuwa walimu wanalipwa mishahara mikubwa sana nchi hii kuliko kada nyingine zote.
Naibu waziri ameyasema hayo kwenye kipindi cha televisheni cha chanel ten.
========
MOSES CHITAMA: Tumekuwa tukipata waajiri ambao ni wakurugenzi kwa mujibu wa sheria ilivyo, mkurugenzi analeta mashtaka kwamba mwalimu huyu amebainika na makosa haya. Tunaanzisha taratibu za kumchukulia hatua za kinidhamu.
Mwalimu anapewa barua ya shtaka ajieleze ambae anaundiwa kamati za uchunguzi kuchunguza shauri lake, Je ni kweli alifanya hayo makosa? Ni kweli alikuwa amelewa? Ni kweli alitukana? Ni kweli alipigana na mwalimu mwenzie eneo la kazi? Ni kweli mwalimu ni mtoro? Ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mwanafunzi?
Ibainike, ithibitike pasipo shaka ni kweli mwalimu alikuwa anafanya mapenzi na mtoto wa shule, ikishabainika sasa hatua za kinidhamu zinachukuliwa. Mwalimu anaweza akafukuzwa kazi na kama alikuwa mtoro, mwalimu mwengine unakuta ametoroka mwaka mzima hayupo kumbe anafundisha private, huku anafundisha private huku anachukua mshahara wa serikali.
MWANDISHI: Kwanini huyu anatafuta kazi ya ziada, inawezekana kipato anachokipata mwalimu huyu ni kidogo?
MOSES CHITAMA: Kati ya walimu ambao wana maslahi mazuri, ambao wanapewa kipaumbele na serikali ni walimu. Mishahara yao mikubwa ya walimu, yaani ukimaliza degree yako unapata mshahara mkubwa kuliko mtumishi mwingine anaeanza, anaemaliza degree yake anaenda kwenye fani zingine. Mwalimu mshahara wake ni mkubwa, sitaki kukwambia hapa ni shilingi ngapi lakini huo ndio ukweli.