Tarehe 16 September 2016 nilisafiri na Basi la Newforce toka Dar to Songea, Safari ilikuwa nzuri sana toka tunaondoka Ubungo, nakumbuka nilikaa seat no A2, A1 alikaa rafiki yangu ambaye alikufa dakika chache baada ya ajali kutokea
Basi hili halikuwa na tatizo lolote maana toka Dsm halikupoteza hata dakika likifanyiwa matengenezo njiani, Sasa mida ya saa mbili tukiwa sehemu ya Kifanya Njombe gari lilimzidi dereva kutokana na kona halafu mteremko, kwa kuwa tulikaa siti ya mbele kabisa dereva alisikika akimwambia conductor wake Cassian huu msala, sitaweza kulirudisha Tena, wakati huo Basi linayumba mwendo mkali na watu wanapiga kelele, kumbuka haya yote ni ndani ya dakika moja tu kishindo kikubwa kikasikika na abiria wote tukajikuta badala ya kukaa tukajikuta tumelala kiubavu ndani ya Basi, wengine wanalia, wengine wamekufa, wengine damu zinawavujia bila kujua zinatoka kwny jeraha la nani
Ajali naifananisha na ambushi, huwezi ukajiandaa kuikabili, rafiki yangu alikufa miongoni mwa 19 waliokufa, ila bado nakumbuka na kumpenda minza wangu kipenzi
RIP minza