Katika hali na mazingira haya, ukimuuliza mbunge wako kwanini yeye halipi kodi kwenye kipato chake, unadhani atatoa utetezi gani ukamwelewa?

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Hii video ina-trend kwa kasi sana kwenye social media platforms mbalimbali WhatsApp, FB, Instagram, Telegram, Twitter nk nk.

Ukweli huu umewakera wengi sana hususani wanapohusianisha na kodi hizi hatari za tozo kwenye miamala ya fedha kupitia mitandao ya simu walizopitisha juzi.
Your browser is not able to display this video.


Kilichonifurahisha zaidi ni jinsi ambavyo mitandao hii ya kijamii WhatsApp, FB, Youtube, Instagram na mingine inavyosambaza habari kwa kasi na kuleta impact kubwa katika jamii na kwa muda mfupi.

Inashangaza polisi kwa kutumiwa na baadhi watawala wajinga na wapumbavu kupambana na watu kama Askofu Emmaus Mwamakula na wenzake huko CHADEMA wanaotembea kote nchini kutoa elimu ya katiba kwa kuonesha mapungufu ya katiba ya 1977 na umuhimu wa kuandikwa kwa katiba mpya ya wananchi.

Niko huku Shinyanga vijijini maeneo ya vijiji vya Mwakitolyo na Salawe. Nilishangaa sana kuona wazee, vijana wa kike na kiume na watoto wakishangaa kusikia kwamba kumbe wabunge ndiyo wako hivi.

Yaani wao wanatutungia sheria za kodi za kutunyonya sisi wananchi huku wao wakijitungia za kujilinda na kujihakikishia ulaji zaidi na zaidi kila siku.

Ingekuwa vyema kama serikali hii dhalimu ya CCM na Samia Suluhu Hassani Rais wao, wangeelekeza nguvu zao kupambana na social media kama alivyofanya Mwendazake ili nao wafe kama alivyokufa mzee wao.

Katika hali na mazingira haya, hivi ukimuuliza mbunge wako unadhani anaweza kutoa utetezi gani wa kueleweka ya kwanini yeye halipi kodi hizi za kijinga walizozipitisha juzi?
 
Atasema waulizwe mamlaka husika za kodi, yeye atakuwa anaingilia mhimili mwingine
 
Jibu lake ni refa na jaji hawaruhusiwi kuwa sehemu ya kesi, atasema akilipa kodi atajipendelea alipe kidogo hivyo ni bora asiwe sehemu ya walipaji!
 
Kuna mmoja nilimuuliza akajibu hata wao wameyakuta tu. CCM huwa inaokota wapi hawa watu,reasoning yao ni extremely poor
 
Kuna haja ya ubunge uwe wakujitolea tu majimbon tupitshe bakuri la yeyote mwenye ela amchangie mbunge wake na sio lazima apo njaa zitawakaa sawa wachumia tumbo ao wanakela hadi sio vizuri nawenyewe wanajua sana kuwa wanakosea sema ndio hivo aliyeshiba hamjui mwenye njaa......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…