MWAISEMBA CR
Member
- Apr 21, 2014
- 87
- 81
Ni ukweli usiopingika hali ya maisha ya watu yamebadilika na imezidi kuwa mbaya zaidi, hali ya uchumi imeporoka sana wala hakuna pa kupumulia, na ni kweli vitu vimepanda bei kuliko mwanzo na Zaidi ya yote wananchi tumetwishwa Msalaba mkubwa wa Kulipia kodi kila huduma tunayoifanya hasa katika TOZO ZA MIHAMALA YA SIMU,MAKATO MAKUBWA KATIKA BENKI NA BEI ZA MAFUTA KUPANDA n.k.Yaani yapo mengi sana ambayo siwezi kuyamaliza yote, ambayo ni haki yetu kabisa Kuilaumu Serikali yetu ya Tanzania
Kimsingi hata mimi siungi mkono haya tunayotendewa maana inatumiza sana sisi wananchi hasa wenye vipato vya chini!!Lakini swali la kujiuliza pamoja, NANI WA KULAUMIWA? NI NANI AMETUFIKISHA HAPA?JE NI MAMA(RAIS), NDIO AMETUFIKISHA KATIKA HALI MBAYA HIVI(Jibu si Kweli)?
Katika hili, la hali ya uchumi kuporomoka na kufikia hapa tulipo, Mimi SIONI HATIA YEYOTE JUU YA MAMA,RAIS SAMIA SULUHU ingawa ni kawaida na ni haki Kuilaumu Serikali iliyopo madarakani kuwa ndio chanzo cha yote.Kwanini nasema Sioni Hatia kwa mama?
Kwanza, Ikumbukwe sio Mama ametufikisha hapa wala sio mtu wa kulaumiwa!! , kwani mama ameipokea nchi na kuwa Raisi akiikuta Nchi tayari IMEPOROMOKA KIUCHUMI, Yaani iko kwenye hali mbaya sana ingawa Enzi zile HATUKUAMBIWA UKWELI wala Hakukuwa na Vyombo vya habari vyenye uwezo wa kutoa taarifa mbaya kama hiyo,Vikabaki salama!Isipokuwa Nchi nzima tuliaminishwa kuwa tumepanda kiuchumi na hadi kufikia Uchumi wa kati na zaidi tuliamini zaidi kwani tuliona kila kona ya Nchi maujenzi ya barabara yanaendelea, maununuzi ya ndege yanaendelea,Ujenzi wa Treni za umeme na Miundombinu nyingi kuongezeka ingawa hivyo sio kipimo sahihi cha uchumi kuongezeka
Mama yetu amekuwa Rais kwa ghafla bila kutegemea baada ya Mtangulizi wake Rais Magufuli kufariki, na kumuachia nchi ikiwa tayari ipo kwenye hali mbaya sana ingawa hatukuelezwa sana hapo mwanzo.Lakini kilichotufanya leo tupige kelele nyingi za kumlaumu Mama ni kwasababu tu yeye alipoingia kwa sehemu amefungulia uhuru wa kuzungumza,kukosoa na uhuru wa vyombo vya habari ambayo, nina uhakika haya tunayoyasema ovyo kwa Rais Samia, au haya yanayoandikwa mitandaoni yasingeandikwa hivi kama angelikuwepo Rais Magufuli hata kama angeyafanya
Kumbuka Rais Magufuli ndiye alipitisha Kulipia vitambulisho vya wamachinga sh 20,000 bila hata kupitishwa na bunge lakini wote tulishangilia,Kumbuka kuna Uvunjifu mwingi na wa wazi ya Sheria na katiba ulifanywa na Rais magufuli kwa madai ya kuwa alikuwa anajenga nchi, lakini bado watu walishangilia, lakini wote tunafahamu jinsi Rais magufuli alivyotumia Tra kuwakandamiza wafanyabiashara na makampuni kulipishwa kodi kubwa na akaunti zao kufilisiwa, wengi waliitwa wahujumu uchumi n.k na viwanda vingi kufungwa na benki kufungwa, lakini bado hakukuwa na kelele kama hizi? JE SWALA LA TOZO LIMEKUWA GENI KWETU KWA SERIKALI ILE ILE YA CCM ILIYOKWISHA KUYAFANYA YOTE KAMA HAYO HUKO NYUMA?
Mimi nafikifi sio Mama wa kulaumiwa, Ikiwa basi tunamtafuta Mchawi basi Mchawi ni mtangulizi wake, Maana yeye(mama) ameipokea nchi ikiwa katika hali hii mbaya na mama hana hata miezi 7 katika utawala wake, alafu tunamtwisha mabaya yote, tukisahau yupo aliyemtangulia aliyetufikisha hapa.? JE UNGELIKUWA WEWE RAIS, UNGELIFANYAJE CHINI YA CCM ILE ILE?
Mimi nafikiri kilichobadilika ni approach tu za kushughulikia matatizo yaliyopo!Rais Magufuli alitumia Nguvu kubwa kuwabana watu wa juu yaani wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda, wawekezaji na taasisi kubwa kubwa kupitia mlango wa Tra kumsaidia kukusanya kodi kubwa kwao iliyopelekea wafanyabiashara wengi kufunga biashara zao, wawekezaji kukimbia nchi, viwanda vingi kupunguza wafanyakazi wao!Ingawa Approach hii haikuonyesha moja kwa moja kumbana Raia wa kawaida na ndio maana tulimsifia sana Rais magufuli kuwa ni Rais wa wanyonge
Lakini,Mama yeye alipoingia alibadilisha tu gia(Approach) ambayo hatukuizoea, kinyume na ya mtangulizi wake, Alikataza Tra kufanya waliyokuwa wanayafanya ya kuwalipisha kodi zisizostahili wafanyabiashara na wawekezaji.Mama yeye hakutaka kuwaumiza watu ambao ingetupasa kuwatumia kutusaidia kuajiri watu zaidi ila bado ikiwa amezuia ile njia iliyomsaidia Mtangulizi wake kupata mapato,Je yeye(mama) afanyaje na atumie njia gani ambayo bado itamasadia kuendesha nchi aliyoikuta tayari ina hali mbaya?
Hii,Ndio maana mama yeye ameona atumie njia aliyoiita Njia shirikishi aliyoiona yeye kuwa inafaa kuwa WOTE TUSHIRIKI TABU HII PAMOJA bila kuwalemea wafanyabiashara, makampuni, wawekezaji kaam ilivyokuwa kabla, Ndipo alipoamua KUTUMIA NJIA YA TOZA kama sehemu ya kumuingizia kipato ili aweze kuongoza nchi aliyoikuta tayari imeshaharibiwa!! Je atakuwa amekosea kutumia njia hiyo? Au wewe ulitaka atumie njia gani?Ukizingatia ni kweli nchi haina fedha za kutosha kuendesha nchi hasa katika kipindi hichi cha janga la Corona?
Hapa wengi wetu, watakimbilia kumlaumu mama kwanini atutumie sisi wananchi kama chanzo cha mapato asitafute vyanzo vingine kama utalii au kutumia maliasili zetu na utajili mwingi tulio nao?.Ni vyema kabisa kufanya hivyo ndio njia nzuri, ila ebu fikiri unafikiri kwanini umlaumu yeye kutotumia hiyo, kwani watangulizi wake wote kwanini hawakuzitumia hizo rasilimali kama vyanzo vya mapato ila still walitumia njia za kuwabana wawekezaji na wafanyabiashara? Ok, nafikiri wakati tunaendelea na kipindi cha mpito, ebu msaidie mheshimiwa Rais namna nzuri ambayo anaweza kutumia hizo rasilimali kumsaidia kupata mapato ya kuendesha nchi.
Jambo la Pili, Mimi sioni hatia juu ya Mama,Rais samia, Kwani Tatizo sio yeye isipokuwa Tatizo ni Mfumo aliokuwepo inaitwa CCM NI ILE ILE.Hata pale ambapo alitamani kurudisha democrasia na uhuru kama inavyopaswa kwa kuanza kuruhusu uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa vyombo vya habari lakini bado kwasababu bado yupo chini ya Mfumo ule ule, CCM ILE ILE, wala usitegemee kupata makubwa tofauti na yale yale kwa mtu yule yule, zitabadilika appriach isipokuwa mfumo utabaki ule ule
CCM ILE ILE ndio iliyomshauri mama kutumia njia hii ya TOZO KWA WANANCHI WOTE ili aweze kuendesha nchi iliyokuwa katika mazingira haya magumu.Ikiwa ni kumlaumu basi Sio kumlaumu Mama,Rais samia bali Tuilaumu CCM ILE ILE ndio imetufikisha hapa tulipo
Pamoja na kwamba Siungi mkono swala la Tozo ambayo inatuumiza sana lakini bado sioni hatia kwa mama kutumia njia hiyo ili kumsaidia yeye na serikali yake.Na Kimsingi nimefurahia kwasababu kupitia kuumizwa huku kwa pamoja kupitia tozo na kupanda bei ya vitu mbalimbali kutatuweka karibu zaidi na kutatufanya tuwe na lugha moja, maana tulikuwa tumegawanyika.Jambo hili ndilo linatufanya hata leo tukiikosoa CCM ILE ILE bado tusikike zaidi na ndio wataelewa nia yetu njema ipo pale pale
Solution ya Tatizo hili, sio kwamba Mama,Rais Samia ana hatia au ni mbaya sana, wala sio kwamba mama anapenda kutuona watanzania tunaumia hivi, ISIPOKUWA TATIZO NI MFUMO ULIOPO SASA NI MBOVU na ukielewa hili ndilo litakufanya Turudi pamoja KUDAI KATIBA MPYA
Bila kuwekeza kudai katiba mpya ambayo itabadilisha misingi na mifumo yote mibovu ya kiutawala na kimaongozi, bado tutajikuta tunazunguka pale pale!Kubadalika kwa Rais hata angekuwa mzuri kiasi kama anaongozwa na mfumo mbovu bado hautaweza kuuona uzuri wake.
Leo hii pamoja wananchi tumelia na kuongea na kutoa maoni yetu ya kukataa tozo lakini Nguvu yetu ya umma haifanya kazi yeyote kwasababu KATIBA iliyopo inampa Nguvu Mtawala au Serikali kutumia Dola kadiri inavyoweza kuamua lolote wanalotaka kuamua kulifanya bila wananchi kuifanya serikali chochote.Wananchi hatuwezi kuiwajibisha serikali yetu kwasababu nguvu kubwa ya maamuzi ipo kwao watawala KATIBA MPYA Ndio njia bora ya kufanyika ili Turudi katika TANZANIA MPYA
🔵Na:Shujaa Charles Richard Mwaisemba(©️®️Ⓜ️)
stmwaisembac@gmail.com
0712054498/0759420202