demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Tumepata kuisikia press ya Boss wetu Mohamed Dewji leo akiongea na vyombo vya Habari. Kilichonishtusha zaidi ni kuhusu ile Bilioni 20 aliyotuahidi wanachama kuitoa mara apatapo nafasi ya kusimikwa kama sehemu ya umiliki wa Klabu yetu. Mpaka sasa Mo ajaitoa hiyo pesa yote, huku akitoa majibu mepesi mepesi kuwa pesa hatoitoa yote kwa sasa na badala yake atatoa bilioni 3 kila msimu.
Kilichonishangaza zaidi ni kumsikia akilalamika kuwa kuna watu ndani ya Simba wana chokochoko. Yaani wanachama tunaanzaje kuwa na chokochoko kwa kuhoji masuala ya msingi?
Mategemeo yetu mpaka sasa tuwe tumeanza kujenga academy ya Simba, cha kushangaza kwenye press akawa anazungumzia habari ya kutufita vipaji mikoani. Sasa hivyo vipaji vitaenda kucheza wapi? Mchangani?
Ni muda sasa umefika viongozi wa klabu yangu tuweke kikao ili tujitafakari na kujadiri kwa kina malengo yetu kama klabu. Huu sio muda wa wanasiasa kufanya siasa zao klabu ili hali wanachama wanataka kuona maendeleo ya kweli.
Ninaamini mimi ni mmoja wa wachache niliyepata ujasiri wa kujitokeza na kuzungumza siuala hili.