elixer of life
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 633
- 624
Mama huyo akashika mimba ya Yesu kwa kushirikiana na Mungu. Ndiyo kusema kwamba Yesu akiwa mwana halisi wa Mungu akazaliwa pasipo kuwa na dhambi, hata hivyo akachukua sifa na sura ya binadamu.KAFARA KWA MWANADAMU:
Ili kutatua tatizo lisiloweza kutatulika kidhahiri, Mungu akawaza mpango wa akili sana.
Haijulikani kwamba yeye alishauriana na mwana ama hapana; ama wote wawili wakawaza mpango huu wakati mmoja; au uliwazwa na mwana peke yake lakini ikakubaliwa na Mungu Baba.
Maelezo ya mpango huu yalifafanuliwa katika zama za Yesu kama ifuatavyo. Miaka elfu mbili iliyopita 'Mwana wa Mungu' aliyeshirikiana na Mungu katika umilele barabara, alipata kuzaliwa tumboni mwa mama wa kibinadamu.
Akiwa 'Mwana wa Mungu' yeye akajikusanyia ndani yake sifa kamilifu za kibinadamu na pia za Mungu Baba.
Tena tunaambiwa ya kwamba mama mmoja mwema na mtawa, jina lake Mariamu, akachaguliwa kuwa mzazi wa 'Mwana wa
Mungu'
Mama huyo akashika mimba ya Yesu kwa kushirikiana na Mungu. Ndiyo kusema kwamba Yesu akiwa mwana halisi wa Mungu akazaliwa pasipo kuwa na dhambi, hata hivyo akachukua sifa na sura ya binadamu.
Hivyo akajitolea kwa hiari yake kubeba mzigo wote wa madhambi ya wale watu watakaomwamini na
kumkubali kuwa mwokozi wao.
Kwa njia ya mpango huo wa akili, inadaiwa, Mungu akaepa kuhatarisha sifa yake ya uadilifu halisi.
Kumbukeni ya kwamba sawa na mpango huu pia mtu hatasamehewa dhambi pasipo kuadhibiwa. Bado Mungu ataweza
kumwadhibu mwenye dhambi bila ya kuepa sifa yake ya uadilifu.
Tofauti yenyewe ni kwamba sasa Yesu ataadhibiwa, siyo wale wana na mabinti wa Adamu waliotenda dhambi. Hiyo ni fidia ya Yesu itakayosababisha kuwaondolea dhambi watoto wa Adamu.
Mantiki hiyo hata ikionekana ya ajabu na ya kutatanisha , lakini ndivyo ilivyokubaliwa hasa kwamba ilitendeka.
Yesu akajitolea mweyewe na akaadhibiwa kwa ajili ya dhambi ambazo hakuzitenda kabisa
KWAHIYO HAPO MUNGU ALIMSHIRIKISHA MWANAADAM SIO dah huu moto unatusubiri wengi sana