Katika hili Wallace Karia amekosea sana

Katika hili Wallace Karia amekosea sana

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2014
Posts
242
Reaction score
676
Je, Wallace Karia yuko sahihi kusimamisha Ndondo Cup? Kwa maoni yangu sidhani kama yuko sahihi.

Kwa kutumia ushabiki wa Simba na Yanga kuna wanao mkubali Shaffih Dauda na kuna wanaomkataa ila tukija kwenye NDONDO CUP sidhani kama kuna mdau na shabiki wa soka Tanzania ambaye atamkataa Shaffih kama yupo basi ana tatizo la kimfumo kichwani.

Ndondo Cup imekuwa msaada mkubwa sana wa kupromote, kukuza na kuwatafutia malisho mazuri wachezaji wasio na mawakala au connection na viongozi wa vilabu vikubwa. Mfano hai ni Idd Nado, huyu ni zao la Ndondo Cup.

Ndondo Cup imesaidia kuuleta mpira wa mtaani kwenye nyuso za wadua wengi soka ambao hawakuwa na muda wa kuutazama au kuufuatilia.

Sasa ni aibu sana kwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi ya soka nchini kuwa chanzo cha kuua platform ambayo imekuwa na msaada mkubwa sana wa kuibua na kuvionesha vipaji vya watanzania kwa wadau wa soka.

Nadhani maamuzi haya ya Karia yametokana na sababu binafsi (person issue) kati yake na Shaffih na wala siyo kwa mustakabadhi wa soka la Tanzania.

Karia alipaswa kuja na mbinu za kuipromote ligi ya mkoa wa Dar ili iwe na ushindani na ubora kuliko ndondo na wala sio kuipromote kwa kudidimiza ndondo.

Alipaswa kutafuta njia sahihi ambazo hazitaathiri ndondo.Sababu alizozitoa kwamba ndondo inapelekea majeraha kwa wachezaji wa ligi kuu ni za kitoto mnoo.Kwanza nani amewalazisha kucheza, majeraha ni sehemu ya soka.Nadhani hii sio sababu ya msingi.

Moja ya njia bora ambayo ingepelekea Ligi ya Mkoa wa Dar kuwa na mvuto ni kutafuta wadhamini,ligi iwe na hela ya kutosha kuliko ile ya ndondo hapo vilabu vya Mkoa wa Dar vingekimbia ndondo na kuja kwenye ligi ya mkoa. Nadhani hii ingekuwa ndio njia bora zaidi.

#Ni_maoni_yangu

View attachment 2137949
IMG-20220303-WA0014.jpg
 
Basi akataze na diwani cups ambazo zinaua mpira wetu.

Huyu jamaa ni janja janja tuu anatamani udhamini wa ndondo waupate tff wanyonye klabu.
 
Idd Selemani 'nado' Misosi-Mbeya city-Azam fc#Taifa stars
Mussa chibwabwa-Misosi-Manzese-lipuli na mpaka now yupo ligi kuu n.k.aseme mengine ndondo katudanganya
 
Hivi ndondo inakuza vipaji kweli??, Tunajua maana kukuza vipaji??.

Ndondo cup ipo kibrudani na wala sio kukuza vipaji, kwahiyo na hao wachezaji wa ligi kuu hucheza ndondo ili wakuzee vipaji??.
 
Hivi ndondo inakuza vipaji kweli??, Tunajua maana kukuza vipaji??.

Ndondo cup ipo kibrudani na wala sio kukuza vipaji, kwahiyo na hao wachezaji wa ligi kuu hucheza ndondo ili wakuzee vipaji??.

Kuna talent nyingi ambazo zinakosa nafasi ya kuonekana ila ndondo ilipata kuwa platform bora ya kufanya waonekane wapate team kubwa
Idd nado
Kelvin sabato kiduku
Mangalo
 
Usiseme wadau wa Soka Tanzania, Sema wadau wa Soka Dar....
Ndondo haijawahi kuza kipaji cha mtu yoyote, maana ni kina Chuji ( ligi kuu players) ndio wanaocheza
 
Hivi ndondo inakuza vipaji kweli??, Tunajua maana kukuza vipaji??.

Ndondo cup ipo kibrudani na wala sio kukuza vipaji, kwahiyo na hao wachezaji wa ligi kuu hucheza ndondo ili wakuzee vipaji??.
Kuna kuwa na kipaji na kuna platform ya kuonekana, ukitumia akili kidogo tu utaona hivi vitu vinategemeana.
 
Ndondo faida yake ni asilimia 10 huku hasara ikiwa ni 90% kwenye soka letu
 
Kuna kuwa na kipaji na kuna platform ya kuonekana, ukitumia akili kidogo tu utaona hivi vitu vinategemeana.
Toka imeanza hebu nitajie hata wachezaji 20 tu walio ligi kuu!!.
 
Usiseme wadau wa Soka Tanzania, Sema wadau wa Soka Dar....
Ndondo haijawahi kuza kipaji cha mtu yoyote, maana ni kina Chuji ( ligi kuu players) ndio wanaocheza
Kwa sababu huifuatilii hivyo huwezi kuijua
 
Hii ndondo watu wanasema inakuza vipaji, hebu tuwataje wachezaji waliotokea ndondo cup tukilinganisha na muda ambao imeshachezwa. Hapa ndio tunaweza kujua ukweli
 
Hapo suluhisho sio kukata ndondo ni kukataza hakuna mchezaji wa timu za ligi kuu kushiriki hayo mashindano basi
 
Back
Top Bottom