DIDAS TUMAINI
JF-Expert Member
- Nov 11, 2014
- 242
- 676
Je, Wallace Karia yuko sahihi kusimamisha Ndondo Cup? Kwa maoni yangu sidhani kama yuko sahihi.
Kwa kutumia ushabiki wa Simba na Yanga kuna wanao mkubali Shaffih Dauda na kuna wanaomkataa ila tukija kwenye NDONDO CUP sidhani kama kuna mdau na shabiki wa soka Tanzania ambaye atamkataa Shaffih kama yupo basi ana tatizo la kimfumo kichwani.
Ndondo Cup imekuwa msaada mkubwa sana wa kupromote, kukuza na kuwatafutia malisho mazuri wachezaji wasio na mawakala au connection na viongozi wa vilabu vikubwa. Mfano hai ni Idd Nado, huyu ni zao la Ndondo Cup.
Ndondo Cup imesaidia kuuleta mpira wa mtaani kwenye nyuso za wadua wengi soka ambao hawakuwa na muda wa kuutazama au kuufuatilia.
Sasa ni aibu sana kwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi ya soka nchini kuwa chanzo cha kuua platform ambayo imekuwa na msaada mkubwa sana wa kuibua na kuvionesha vipaji vya watanzania kwa wadau wa soka.
Nadhani maamuzi haya ya Karia yametokana na sababu binafsi (person issue) kati yake na Shaffih na wala siyo kwa mustakabadhi wa soka la Tanzania.
Karia alipaswa kuja na mbinu za kuipromote ligi ya mkoa wa Dar ili iwe na ushindani na ubora kuliko ndondo na wala sio kuipromote kwa kudidimiza ndondo.
Alipaswa kutafuta njia sahihi ambazo hazitaathiri ndondo.Sababu alizozitoa kwamba ndondo inapelekea majeraha kwa wachezaji wa ligi kuu ni za kitoto mnoo.Kwanza nani amewalazisha kucheza, majeraha ni sehemu ya soka.Nadhani hii sio sababu ya msingi.
Moja ya njia bora ambayo ingepelekea Ligi ya Mkoa wa Dar kuwa na mvuto ni kutafuta wadhamini,ligi iwe na hela ya kutosha kuliko ile ya ndondo hapo vilabu vya Mkoa wa Dar vingekimbia ndondo na kuja kwenye ligi ya mkoa. Nadhani hii ingekuwa ndio njia bora zaidi.
#Ni_maoni_yangu
View attachment 2137949