Wewe unaona ukimrudisha kwao umemsaidia nini, kwa nini aliyempa mimba asipatikane akaozeshwa?Kwa hiyo ushauri wako ni kumlea huyo binti na mwanae atayemzaa, au kumpa pesa za kwenda kutoa mimba badala ya nauli ya kurudi kwao, au kuacha kuajiri mabinti toka vijijini kwa ajili ya kazi za ndani?
Sijakuelewa!!!!
Kwa hiyo ushauri wako ni kumlea huyo binti na mwanae atayemzaa, au kumpa pesa za kwenda kutoa mimba badala ya nauli ya kurudi kwao, au kuacha kuajiri mabinti toka vijijini kwa ajili ya kazi za ndani?
Sijakuelewa!!!!
Ninacho maanisha ni hiki, ebu tafakari mtoto katoka familia masikini, anakuja kwako kujikwamua na umasikini, bahati mbaya anapata ujauzito, badala ya kumbana kumtaja aliyempa huo ujauzito, badala yake hakina mama wanacho fanya ni kumpa kipigo kama mwizi, kisha kumrudisha kwao,Masaki hata mimi pia sijamwelewa jamaa kabisa yaani alikuwa nalenga nini? Kaitaba please hebu tufafanulie ili tuelewe zaidi.
wakati ukimchukua ulimchukua kama mfanyakazi au ulimchukua ili uwasaidie wazazi wake au umsaidie yeye?..hueleweki.Ninacho maanisha ni hiki, ebu tafakari mtoto katoka familia masikini, anakuja kwako kujikwamua na umasikini, bahati mbaya anapata ujauzito, badala ya kumbana kumtaja aliyempa huo ujauzito, badala yake hakina mama wanacho fanya ni kumpa kipigo kama mwizi, kisha kumrudisha kwao,
Sasa angalia, kwao ni masikini halafu anarudi kwao na mzigo, wewe unafikri wazazi watakuonaje,
Njia nzuri ni kumuozesha tu, na mimba wasiitoe anaweza kupata matatizo ukafungwa
namaanisha hilo.
niulize tena
Mimi nakubaliana na wewe, pia na wengine hata kama hawatakubali hapa lakini ukweli unabaki ulivyo, wewe ni kichwaNafikiri hili suala inabidi tuliweke ktk mazingira ya kitanzania yaani tunawachukua hawa watoto wa kike kama wafanyakazi wa ndani lakini kiukweli huwezi kusema ni wafanyakazi per say. Wengi wao unakuta wadogo au hata kama wakubwa mambo mengi hawajui so ni kama kuwasaidia.
Kwa hiyo kwa uungwana unaweza kumsaidia kwamba ajifungue huyo mtoto lakini wazazi wake wataarifiwe kuhusu hali ilivyo na pia lazima amtaje aliye mpa uja uzito, ili mambo ya kiseria yafuate baada ya kujifungua.
Akisha jifungua kama utaona bado anafaa kuendelea kufanya kazi mimi sioni tatizo kwa nini asiendelee kuwepo mpaka yeye aseme anataka kuacha kukaa kwangu. Haya ni mawazo yangu na nafikiri ndivyo inapaswa kuwa.
Unakwenda kijijini unakuta familia masikini sana, hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kutwa, kuwaonea huruma unachukua binti yao hadi kwako mjini akufanyie kazi za ndani, apate pesa awasaidie wazazi wake
Binti akiwa kwako anapata ujauzito, bila kujali ameupata wapi, wewe unamludisha kwao,
-Je! huu ni uungwana?
-Hauoni kuwa unaiongezea familia umasikini na mzigo wa kulea mimba na hatimaye mjukuu?
-hakuna njia nyingine ya kumsaidia huyu binti zaidi ya kumrudisha kwao?
-Je ukikuta mimba hiyo ni ya mwanao wa kiume? na wakati huo umeisha mrudisha kwao!
hivi ukimuuliza mimba kapata wapi na akataja ya mumeo bado utaendelea kukaa nae na kumsaidia?
kwa swala la mshahara ni kweli halina mvuto 15,000.00 ni ndogo sana
Unakwenda kijijini unakuta familia masikini sana, hawana hata uwezo wa kupata mlo mmoja kutwa, kuwaonea huruma unachukua binti yao hadi kwako mjini akufanyie kazi za ndani, apate pesa awasaidie wazazi wake
Binti akiwa kwako anapata ujauzito, bila kujali ameupata wapi, wewe unamludisha kwao,
-Je! huu ni uungwana?
-Hauoni kuwa unaiongezea familia umasikini na mzigo wa kulea mimba na hatimaye mjukuu?
-hakuna njia nyingine ya kumsaidia huyu binti zaidi ya kumrudisha kwao?
-Je ukikuta mimba hiyo ni ya mwanao wa kiume? na wakati huo umeisha mrudisha kwao!
aah leo JF inanifanyia kiini macho 😡
hivi kwa mfano ukimuuliza mimba katoa wapi akakwambia ni ya mmeo utafanya nini hapo??
swala la mshahara nalo ni issue 15,000.00 ni ndogo sana kwa maisha ya sasa sijui huwa tunafikilia nn kuwapa mshahara mdogo namna hii?