Hili sio suala dogo la kukurupuka,Inategemea na kipato cha mtu kikoje,kama wewe mwenyewe haujitoshelezi utawezaje kumhudumia mjamzito na akishajifungua na mwanae?Makubaliano yalikuwa ni kufanya kazi.
Na huo mshahara mdogo wa 15 elfu pia inategemea na kipato cha mtu,kuna wengine ni mabaamedi wanalipwa hela ndogo kwa mwezi.
Ndiyo maana nasema tuchukulie mazingira ya tanzania na nchi nyingine maskini ili tuhusishe utu. Hata hao ma-baa medi kama uliyo sema kuna sehemu wanalipwa vyema na wanaishi ki-vyao lakini kuna sehemu zingine wana mshahara mzuri na wanapewa vyumba vya kulala, hii inatokana na roho nzuri ya mwenye biashara.
Wito wa mtoa mada hii kwa jamii ni kwamba akina mama/baba tuwe na moyo wa utu na huruma ktk kuishi na watumishi wetu wa ndani na wanapo kosea tuwashauri/tuwaadhibu kama ndugu zetu/watoto wetu au wadogo zetu.