Katika ile zawadi tuliyo kununulia, kuna jero yangu Father

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Wiki iliyopita baba Paroko wa parokia yetu aliagwa rasmi. Amekuwa Paroko kwa miaka mitano.
Kanisa letu pia lina miliki shule ya msingi pembeni yake. Alhamisi Misa hujumuisha watoto wa shule na waumini lakini watoto wanaongoza kila kitu pamoja na kusoma masomo.
Maandalizi ya sherehe ya kumuaga Paroko yalihusisha wazazi, walimu, wanafunzi na waumini. Kila mtu alitoa alichoweza na waumini walipika vyakula vyao vya asili.

Katikati vya sherehe wakati risala inasomwa. Mwanafunzi mmoja wa miaka mitano alisimama na kwasauti alisema “ Fr Anthony katika zawadi ya darasa la kwanza nilichanga shilingi 500”.

Wote tulibaki tunacheka, mtoto yule amejitengenezea umaarufu mkubwa kanisani. Waumini tutalikumbuka tukio hili kwa muda mrefu.
 
safi, bila shaka father Anthony alifurahi...atamkumbuka huyo mtoto.
 
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
 
mi sipendi mambo ya kutiana aibu
ningeondoka muda huo huo
 
Back
Top Bottom