Ndugu zangu,
Kwanza napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai kwa kuiona siku ya leo.
Nikirejea katika ile hadithi ambayo mwl Nyerere aliwahi kuisimulia dhidi ya vijana waliokuwa wanataka kuposa binti mzuri sana aliyekuwa anakaa milimani, njia ya kuelekea nyumbani kwao kulikuwa na bibi kizee ambaye alikuwa anawapa tahadhari hawa waposaji dhidi ya sauti ambazo watakuwa wanazisikia kuelekea kule, ila wasizijari bali wazidi kusonga mbele tu. Napia aliwaonya kwa kadiri watakapokuwa wakizidi kusogea, ndivyo sauti zitakuwa zikizidi kuongezeka. Baadhi ya sauti hizo zilisikaka kama ifuatavyo: “huyo huyo, mchinje mchinje, huyo”. Katika hadithi hii mwl alisema: “wewe kazana kwenda mbele tu, usigeuke nyuma, na ukikosea ukageuka nyuma, utageuka na kuwa jiwe”. Basi waposaji wengi sana walitishwa sana na zile sauti, na wengi wao waligeuka wakawa mawe. Ila kuna kijana mmoja hakuzijari hizo sauti alipambana akafika mpaka mwisho na akamposa huyo binti mzuri.
Nini mantiki au kiini cha hadithi hii? Mwl alisema, “katika mambo haya ya kujenga nchi, shabaha kubwa kama hizi, za kuleta haki, za kuondoa dhuluma, za kuleta haki katika dunia, mnajipa shabaha kubwa kabisa”. “Tunataka kujenga nchi ambako hakuna dhuluma dhuluma, safari yake ni ngumu sana, na katika nchi ile itakayokuwa inaonyesha juhudi hizo, itakuwa inasikia sauti hizo, hao hao wamepotea njia hao, wachinje hao ” Miongoni mwa sauti hizi: “zingine zinatoka nje ya Tanzania, na zingine zinatoka hapa hapa Tanzania” Ama tulikusudia kweli ama tulitania, kujenga nchi ya haki au tulikuwa tunatania tu? Kama tulikusudia, hatuwezi tukarudi nyuma kwa kelele za wapumbavu na wanyonyaji…………… Tutapata:
(nimeambatinisha hotuba)
Hicho ilikuwa kipindi ambacho mwl alikuwa anapambana kuinua uchumi wa taifa hili na akawa anapitia kipindi kigumu sana. Hatidhi hii na kiini hiki kimetimia katika kizazi chetu na hasa katika juhudi za kuijenga Tanzania, chini ya uongozi mahili wa Mh. Raisi Magufuli. Katika
kila hatua ambayo Mh. Raisi amechukua ili kuuinua uchumi wa taifa hili, kumekua na kelele nyingi sana tangia aingie madarakani. Zingine zilitoka nje ya Tanzaniana zingine hapa hapa Tanzania (just mfano mmoja tu, dogo alikuwa upande wa mabeberu sana kipindi cha makinikia), lakini Mh. Aliziipuza, na akawaacha waliotaka kugeuka kuwa mawe, akasonga mbele na hatimae AKALIINGIZA TAIFA KWENYE UCHUMI WA KATI.
Katika kipindi cha kupambana na janga la KORONA, Mh. Raisi kwa kutumia washauri wenye hofu ya Mungu, aliamuru taifa tuingie katika maombi ya kufunga ya siku tatu pamoja na kumshukuru Mungu, akaachana na njia za nchi mbalimbali ambazo zinatumia hadi mpaka leo, LOCKDOWN. Kwa unyenyekevu huu mbele za mwenyezi Mungu, Mungu alituepusha na janga hili mpaka leo watu tunaishi kama kawaida.
Katika mapambano ya janaga hili, zilitoka kelele nyingi sana, zingine zilitoka nje ya Tanzania (tutakuwa tunaona maiti zinazagaa mitaani) na zingine ndani ya Tanzania (wapinzani, mfano Mbowe et al.,walitaka lockdown) ila Mh. Raisi alizipuuza tukasonga mbele, hadi leo tunaendelea na maisha kama kawaida. Katika janga hili, Mh. Raisi kwa Neema kuu ya Mungu hatimae alikuwa mshindi dhidi ya kelele hizi.
Nilisikia kipindi dogo anaogea na media za Kenya alisema “Tanzania kuna korona watu wanakufa hovyo tu hakuna social distancing” Lakini huyu huyu dogo kwenye mikutano yake kile alichokisema akiwa Kenya, wala hakitekelezi hapa Tanzania. Jamaa huyu ni miongoni mwa wanasiasa wanafiki sana. Unaenda kwenye taifa jirani ili kuongea kwa nia ya kulichafua taifa, lakini ukiwa hapa wala suala hilo huliongelei. Huyu dogo anajua kabisa kuwa, kwa juhudi ambazo Mh. Raisi alizichukua dhidi ya Korona, zililiokoa taifa hili, ila kwa vile ana chuki naye lazima amchafue tu.
Katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, kuna haja kubwa sana ya kuendelea kumuomba Mungu pia, ili atuvushe salama. Taifa saizi limeshaingiliwa, na viashiria vimeshaanza kuonesha kwa baadhi ya wagombea uraisi, ambao inaonyesha wameshaandaliwa kwa ajili ya kuleta vurugu. Kunawagombea washeanza kusema, saizi hawatamwachia Mungu, tafsri yake ni kuwa, wamemuona Mungu hawezi wanatataka watumie njia zozote zile ili kuleta vurugu na taharuki katika nchi. Ila, naamini kwa nguvu ya maombi, Mungu atatuvusha katika hili pia. Kama ilivyokuwa kwenye juhudi za kuliinua taifa kiuchumi, kupambana na Korona, Mungu alituvusha, na katika hili, naamini Mungu atawaibisha vibaraka hawa na kutuvusha salama.
Nahitimisha kwa kusema, katika juhudi za kupambana ili kuwa na uchumi imara wa kutokuwa na utegemezi, juhudi alizozichukua na ataendelea kuzitekeleza Mh. Raisi ndo zinatakiwa kuwa ndo za kufanya kama taifa huru. Kutatokea na changamoto nyingi sana katika safari hii, zingine zitaletwa na watu wa nje ya Tanzania, na wengine watakuwa watanzania wenyewe wanaogeuka na kuwa vibaraka, Ila lazima tusimame imara kama taifa kwa kumuomba Mungu, ili aendelee kumpa hekima Mh. Raisi ya kulingoza taifa hili kwa miaka mingine mitano.
Asante sana,
Nawasilisha
Kejuu

- Matatizo
- Tutapata majizi humu humu
- Tutapata wanyang’anyi humu humu
- Tutapata watetezi wa mabepari humu humu
- Watazidisha kelele