Katika kosa kubwa ambalo Biden atalifanya ni kuhusu uamuzi wa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu

washirika walikua wanasubiri US afanye kuruhusu tu nao wafuate UK FRA GER soon nao wataruhusu matumizi ya storm shadow. LITHUNIA nayo imeruhusu.
1731929005564.png
 
washirika walikua wanasubiri US afanye kuruhusu tu nao wafuate UK FRA GER soon nao wataruhusu matumizi ya storm shadow. LITHUNIA nayo imeruhusu.
View attachment 3155310
Unaweza ukadhani ni rahisi kiasi hicho,lkn ukweli ni kujiingiza kwenye shimo la kiboko.
Urusi anazo silaha za kufika Kila mji wa NATO atqkaotaka kufikisha,namaanisha kupiga.
 
Biden ameondoa marufuku kwa Ukraine kutumia makombora ya Marekani kushambulia ndani ya Urusi

Joe Biden ameiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa makombora ya masafa marefu ya Marekani.

Rais Biden ameidhinisha Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zinazotolewa na Marekani ndani ya Urusi kwa mashambulizi machache, maafisa wa Marekani wamesema.

Ukraine inapanga kufanya mashambulizi yake ya kwanza ya masafa marefu katika siku zijazo, duru zilisema, bila kufichua maelezo kutokana na wasiwasi wa kiusalama.

Hatua hiyo ya Marekani inajiri baada ya miezi kadhaa ya ombi la Volodymyr Zelenskyy kuruhusu jeshi la Ukraine kutumia silaha za Marekani kushambulia maeneo ya kijeshi ya Urusi mbali na mpaka wake.

Mabadiliko hayo yanafuatia Urusi kupeleka wanajeshi wa nchi kavu wa Korea Kaskazini ili kuongeza vikosi vyake, jambo ambalo limezua taharuki mjini Washington na Kyiv.

Mashambulio ya kwanza ya kina huenda yakatekelezwa kwa kutumia roketi za ATACMS, ambazo zina masafa ya hadi maili 190, kulingana na vyanzo.

Kwa Mtazamo wangu nikwamba sasa hii vita inakuja kuwa vita ya ukanda ambayo italeta maafa makubwa sana labda na sema labda kwa rais mpya atakayeingia apige marufuku kuendelea kutumia Siraha za masafa marefu vinginevyo mambo yatakuwa magu sana!

View attachment 3155252
Mbona urusi wao wanatumia silaha za aina hiyo? Ukraine kuzitumia ndio inaonekana nongwa?
 
Unaweza ukadhani ni rahisi kiasi hicho,lkn ukweli ni kujiingiza kwenye shimo la kiboko.
Urusi anazo silaha za kufika Kila mji wa NATO atqkaotaka kufikisha,namaanisha kupiga.
Huyu Urusi unae msema hapa kila mtu alikua anamwona ni dude kubwa kabla ya vita lakini baada ya gem kuanza had leo kashindwa kukomboa Oblast ya Kursk
 
NATO wanapambana na Rusia wapi?

Kiufupi hii vita ni kama Ukrain kafungwa mikono,
Wanachofanya nato ni kumpa Ukrain silaha kadhaa huku matumizi yake nayo yakiwa ni ya masharti, huku yeye Putin akijipigia tu popote ndani ya Ukrain.

NATO wangeamua kupambana na Putin hiyo vita saa hii ingekuwa ilishaisha
Swala sio vita kuisha Issue ni vinaishaje???Wazungu sio wajinga waharibu maisha yao kisa wanataka kujionesha wana nguvu.
 
Subirini Muda umefika Kyev itakuwa majivu soon leteni mzaa! Pia ikumbukwe hii kitu haitatokea siku akithubutu huyo Zelensky supersonic zitashushwa hapo ukrine bila hata yakujali zinaangukia wapi! maana hapo hakutakuwepo na kitu kinaitwa Hak za binadamu!
 
Biden ameondoa marufuku kwa Ukraine kutumia makombora ya Marekani kushambulia ndani ya Urusi

Joe Biden ameiruhusu Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa makombora ya masafa marefu ya Marekani.

Rais Biden ameidhinisha Ukraine kutumia silaha za masafa marefu zinazotolewa na Marekani ndani ya Urusi kwa mashambulizi machache, maafisa wa Marekani wamesema.

Ukraine inapanga kufanya mashambulizi yake ya kwanza ya masafa marefu katika siku zijazo, duru zilisema, bila kufichua maelezo kutokana na wasiwasi wa kiusalama.

Hatua hiyo ya Marekani inajiri baada ya miezi kadhaa ya ombi la Volodymyr Zelenskyy kuruhusu jeshi la Ukraine kutumia silaha za Marekani kushambulia maeneo ya kijeshi ya Urusi mbali na mpaka wake.

Mabadiliko hayo yanafuatia Urusi kupeleka wanajeshi wa nchi kavu wa Korea Kaskazini ili kuongeza vikosi vyake, jambo ambalo limezua taharuki mjini Washington na Kyiv.

Mashambulio ya kwanza ya kina huenda yakatekelezwa kwa kutumia roketi za ATACMS, ambazo zina masafa ya hadi maili 190, kulingana na vyanzo.

Kwa Mtazamo wangu nikwamba sasa hii vita inakuja kuwa vita ya ukanda ambayo italeta maafa makubwa sana labda na sema labda kwa rais mpya atakayeingia apige marufuku kuendelea kutumia Siraha za masafa marefu vinginevyo mambo yatakuwa magu sana!

View attachment 3155252
Sasa vita inapokuwa stalemate, maafa kutokana na kufa kwa askari yanakuwa mengi na mwishowe Ukraine ataishiwa na askari kutokana na population yao kuwa ndogo. Ni ujinga kuisaidia Ukraine isishindwe vita na hapo hapo kutokuisaidia ishinde vita. Ni vyema kuamua moja tu ili kupunguza hasara.
 
Subirini Muda umefika Kyev itakuwa majivu soon leteni mzaa! Pia ikumbukwe hii kitu haitatokea siku akithubutu huyo Zelensky supersonic zitashushwa hapo ukrine bila hata yakujali zinaangukia wapi! maana hapo hakutakuwepo na kitu kinaitwa Hak za binadamu!
Hakuna silaha ambayo Putin hajaitumia ndani ya Ukraine ukiondoka Nuclear, kwahiyo hautakuwa na jipya ni wakati wa raia wa Urusi kuonja joto ya Jiwe.
 
Back
Top Bottom