Katika kosa kubwa ambalo Biden atalifanya ni kuhusu uamuzi wa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu

Katika kosa kubwa ambalo Biden atalifanya ni kuhusu uamuzi wa kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za masafa marefu

Na kadiri ya sheria za komataifa, taifa linapaswa kudhibiti jirani zake, hasa kufuatilitilia mienendo yake ya kijeshi.
Kabla ya US kutuma 'vijana' wao Kursk, Biden alisema hadharani kuwa ataona namna ya kupambana na uchumi wa Urusi.

Mpngo wa Kursk umebuma ndio amesaini huu, huku akijua anaondoka ikulu na chama kimepoteza ushawishi kabisa kwa raia.
Na ndio anazidi kukipoteza chama chake
 
Subirini Muda umefika Kyev itakuwa majivu soon leteni mzaa! Pia ikumbukwe hii kitu haitatokea siku akithubutu huyo Zelensky supersonic zitashushwa hapo ukrine bila hata yakujali zinaangukia wapi! maana hapo hakutakuwepo na kitu kinaitwa Hak za binadamu!
1000032726.jpg

Mwaka wa ngapi huu
 
Kauli ya kijinga sana hii,hii ni kauli ya kukalili,sio kauli inayotoka kichwani mwa mtu mwenye afya ya akili.
Hivi na Mimi nikisema Ukraine inawajibika kuishi vizuri na jirani yake utaipokeaje kauli hii.
Ni "kariri" na siyo kalili. Hebu hariri hapo juu tuendelee kufikiri pamoja.
 
Kwamba NATO wangekuwa wamesha mmaliza Russia sindio unavyotaka tuamini au !?

Acha ujinga ingekuwa ni rahisi hivyo unavyodhani kinacho wafanya NATO wasiivamie Russia nini mpaka Leo hii , mbona Kwa sadam husen na gadafi waliingia bila kusita umeshajiuliza sababu inayo wafanya wasiingie front kama alivyo fanya Korea kaskazini ni ipi ??

Wanaujua mziki wa Russia , Russia sio Syria mdogo wangu
Dogo Acha ushabiki maandazi!

West wanampukuchua Putin mdogo mdogo mapaka ataisha!

Vita ni akili, Putin aliingia kichwa kichwa ila wenzake wanambonda kwa akili.

Kwanza itafika hatua uchumi wake utasinyaa kabisa na hapo ndipo wanapopataka West.

Vita ni hela sasa hivi Putin anawaza kila shilingi itabidi aitumbukize kwenye vita na hapo ndio mtego kwa Putin ulipo.
Huwezi kuona kwa sasa ila subiri miaka 5 au 6 ijayo uone mziki wake

West wasingejihangaisha kuitumbukiza Ukrain kwenye vita visivyo na maslahi kwao.

Usiwe mburura
 
Kama kawaida yako unapenda kuongea ushabiki na mihemko.
Ulaya nzima hadi Marekani hakuna anayeweza kuikabili Russia hakuna.
Kwa taarifa yako kuna askari kibao wamepenyezwa wa NATO ndani ya jeshi la Ukraine ili waisaidie Ukraine lakini still bado wanapigwa.
Hiyo NATO yenyewe imeundwa kukinzana na vitisho vya Russia.
Narudia tena Ulaya hakuna taifa la kusimama na Russia hata hao NATO hawana huo ubavu.
Mbona Ukrain mwaka wa pili huu na bado wanahenyeka mpaka kuna sehem ya Urusi iko mikononi mwa Ukrain?

Umenikumbusha zile za Hezbollah siyo Hamas
 
North Korea wamo ndani ya jimbo la Kursk ambalo limo ndani ya Russia. Huko mbele maeneo yananyakuliwa na wanajeshi wa Russia wenyewe.

Kama haufahamu viongozi wengi ndani ya Russia hawapendezwi na Putin jinsi anavyoiendesha hii anayoiita SMO dhidi ya Ukraine. Wengi wanataka waharibu kila kitu hapo Ukraine kama Israel anavyofanya Gaza.

Wametoa sababu zao kwa Putin kuwa kwa jinsi tunavyoenda na SMO ni ngumu kumaliza hili sakata. Inabidi tupige na tufanye jambo moja la kikatili litakalomfanya Ukraine asalimu mwenyewe amri kuliko wewe Putin unavyoilea.

Kuna kipindi Putin alienda kutembelea kambi moja ya jeshi nchini mwake moja ya maswali ambayo wanajeshi waliyokuwa wanamuuliza ni kipi kinamfanya asiruhusu jeshi la nchi lisitumie zana zote za jeshi walizonazo kama Ukraine na washirika wake wanavyopambana dhidi yao? Putin akatoa majibu anayoyajua mwenyewe ya kuonyesha uungwaana!

Ila yote juu ya yote wachambuzi wa masuala ya kivita wanasema ili Ukraine na west waache kuisumbua Russia pale Ukraine inambidi Russia ifanye maamuzi magumu ya nguvu yake ya kijeshi ili imlazimishe Ukraine asaini makubaliano mwenyewe ya amani. Mpaka sasa Russia katumia 18% za uwezo wake wa kijeshi.

Hatujui Russia atachukua maamuzi gani, wao wenyewe ndiyo wanajua ikiwa Ukraine ikianza kuitumia hiyo ruhusa waliyopatiwa.
Zana zipi Rusia hajatumia ukiacha nukes?

Mpaka anaomba makombora kwa Iran na Kiduku alafu unasema zana ambazo hajatumia?
 
Hapo ndio Ukraine 🇺🇦 ilipoingia Choo cha Kike.

Ni bora US amfididie Ukraine Mabomu yake ya Nyukilia.

Ila Biden Mungu anauona. Yaani anamdanganya mwenzake ampige jitu, wakati anajua hatakuwepo. Ukraine asipojiongeza, akampiga kweli. Anaenda kufa. Watampiga kipigo cha mbwa mwizi
 
Ila Biden Mungu anauona. Yaani anamdanganya mwenzake ampige jitu, wakati anajua hatakuwepo. Ukraine asipojiongeza, akampiga kweli. Anaenda kufa. Watampiga kipigo cha mbwa mwizi
Putin aache kuua raia,jana nilikuwa naangalia akipiga miundombinu ya kiraia.

Russia alisema atamchakaza Ukraine ndani ya wiki moja tu na hakuna silaha ambayo hajaitumia mpaka kufikia kukodisha Askari kutoka Korea Kaskazini.

Kwahiyo zitapigwa tu Ukraine imethibitisha ubabe wa Mrussi ulikua ni zamani sasa hivi sharubu zake zinashikwa tu nakusokotwa na kupigwa vibao😁
 
Anataka kuhakikisha kuwa mpaka anakabidhi madaraka amemwaribia trump kwa kiasi kikubwa kadri awezavyo.
Bado hujaona hapa mpaka anakabidgi madaraka anataka kuacha kateua hadi majaji..
Mahakama kuu tayari ina majaji wametosheleza...na kule huwezi kuwabadili labda mambo matatu
1.Jaji Afariki
2.Jaji astaafu
3.jaji afanye kosa litakalomuondolea sifa ya kuwa jaji...

Vinginevyo hakuna kitu anaweza kufanya...
 
Back
Top Bottom