Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Wakuu,
Embu tuambiane ukweli hasa kwa sisi vijana, kweli ushawahi kuona mtu anatoa rushwa au anakuomba kitu kidogo ukaenda kuripoti kuwa umeombwa Rushwa?
Ukiangalia wanaokula mabilioni hawakamatwi, sasa kwanini umchome huyu anayetaka buku kumi au elfu 50 wakati anakufanyia jambo lako fasta na kila mtu anafaidika? Yaani nifike sehemu najua nikitoa buku 10 mambo yanaenda fasta halafu niende kumripoti, wakati akidakwa hilo jambo la saa moja linaweza kuchukua hata wiki?
Soma,Pia: Mapambano dhidi ya Rushwa katika Miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Samia
Kama wale papa wasipoadabishwa watu wanapolalamika nini kitabadilika kuripoti huyu dagaa ambaye ukute naye yupo kwenye mazingira magumu sababu ya mkubwa wake? Kwenda kuripoti inakuwa kama kupoteza muda tu! Au nasema uongo ndugu zangu?🌚🌚
=====
Julai 11 ilipitishwa na Umoja wa Afrika (AU) kuwa Siku ya Mapambano dhidi ya Rushwa Barani Afrika. Kwa mwaka 2025, maadhimisho haya yamebeba kaulimbiu “Kudumisha Hadhi ya Binadamu katika Mapambano Dhidi ya Rushwa Barani Afrika.”
Kaulimbiu hii inaendana kikamilifu na kaulimbiu kuu ya Umoja wa Afrika kwa mwaka 2025 “Haki kwa Afrika na Watu wa Asili ya Kiafrika Kupitia Marekebisho na Maridhiano (Reparations).”
Rushwa inaporomoa haki, hadhi na maendeleo ya watu. Kupambana nayo si jukumu la serikali pekee bali ni la kila mmoja.