Uchaguzi 2020 Katika kufungua kampeni jana nimemshuhudia mgombea kupitia CCM John Pombe Magufuli akiwa mtulivu na mnyenyekevu sana

Uchaguzi 2020 Katika kufungua kampeni jana nimemshuhudia mgombea kupitia CCM John Pombe Magufuli akiwa mtulivu na mnyenyekevu sana

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Katika kufungua kampeni jana nimemshuhudia mgombea kupitia CCM John Pombe Magufuli akiwa mtulivu na mnyenyekevu sana.Pia kwa mara ya kwanza kwa muda wote wa hotuba yake alikuwa akitumia “tuaomba miaka mitano tena” na sio naomba miaka mitano tena (ameondoa u mimi ambao amekuwa akiiutumia kwa takribani miaka mitano sasa.Kama mabadiliko haya ni kwa ajili ya kampeni tu,hakuna ajuae ila kwa kweli tuvute subira.

Pamoja na hayo hakuacha jadi yake ya kutia mzaha hata pasipostahili kwa sifa alizompa Mama Samia,nahisi ni udhaifu wake tumvumilie.Ameyataja mafanikio yake makubwa katika vitu vinavyoshikika na kuonekana na kwa hili pongezi nyingi sana.

Jambo ambalo halikulisikitikia ni pamoja na yaliyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ambayo yanaelekea kutokea tena katika uchaguzi mkuu huu.

Wakati ambapo tunawaza kumpa tena miaka mitano mingine ni lazima tutafakari kauli ya Ndugai ya kutaka CCM wawe na 2/3 ya wabunge ili waweze kufanya watakalo.Ni jambo la hatari mno na deep root state (Serengeti wameweza)watusaidie kuhakikisha kuwa hila hazitumiki kulifanikisha hilo kwa mustakabali mwema wa nchi.

Tulishaishi kama Chama Kimoja na faida na hasara tuliziona tusirudi tena huko,tuipalilie demokrasia ikue na tuongeze uhuru wa watu wetu.
Kampeni njema,amani na usalama wa watu wote uwe kipaumbele chetu.
 
Hiyo ni lugha ya campaign tu. Na hua haiondoi nature ya mtu.
Utulivu huo lakini mtu haahidi uhuru wa kujieleza, democracy ya kweli na katiba mpya ya wananchi iliyokwama ?!.
 
Kwahiyo hapo ndo umechambua siasa au🤔? Mkuu hebu jaribu kuchambua karanga Kama Saida karoli, huenda ukafanikiwa.Watu wengine bn 😁.
 
Mradi wa SGR pekee unatosha kuniambia kuwa Magufuli ana mpango kabambe wa kuongeza muda.

Dalili kuu ya kwanza ni kuenguliwa wagombea wa upinzani Pemba. Hili ni janga tunachuma.
 
Hayo ni yale machache ulosikia ,japo kaongea mengi ya maana na muhimu.
 
Hivi jana aligusia kuhusu maslahi ya watumishi wa umma?
 
Hivi jana aligusia kuhusu maslahi ya watumishi wa umma?
Natamani nimsikie tena akiwaambia wale akina IWE BHOJOO, kuwa sio yeye aliyeleta tetemeko. Akiwaambia tena wale watu wa Mwakata Kahama kuwa, serikali haitawajengea nyumba zilizosombwa na mafuriko, ambazo aliyekuwa Rais wakati huo aliahidi JKT ingewajengea.
 
Je aliongelewa kuhusu udhaifu wa NEK ??

Hiyo ndio burning issue
 
Kwahiyo hapo ndo umechambua siasa au[emoji848]? Mkuu hebu jaribu kuchambua karanga Kama Saida karoli, huenda ukafanikiwa.Watu wengine bn [emoji16].
Wasomaji wa uchambuzi wako wapi?
 
Back
Top Bottom