Katika kufungua kampeni jana nimemshuhudia mgombea kupitia CCM John Pombe Magufuli akiwa mtulivu na mnyenyekevu sana.Pia kwa mara ya kwanza kwa muda wote wa hotuba yake alikuwa akitumia “tuaomba miaka mitano tena” na sio naomba miaka mitano tena (ameondoa u mimi ambao amekuwa akiiutumia kwa takribani miaka mitano sasa.Kama mabadiliko haya ni kwa ajili ya kampeni tu,hakuna ajuae ila kwa kweli tuvute subira.
Pamoja na hayo hakuacha jadi yake ya kutia mzaha hata pasipostahili kwa sifa alizompa Mama Samia,nahisi ni udhaifu wake tumvumilie.Ameyataja mafanikio yake makubwa katika vitu vinavyoshikika na kuonekana na kwa hili pongezi nyingi sana.
Jambo ambalo halikulisikitikia ni pamoja na yaliyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ambayo yanaelekea kutokea tena katika uchaguzi mkuu huu.
Wakati ambapo tunawaza kumpa tena miaka mitano mingine ni lazima tutafakari kauli ya Ndugai ya kutaka CCM wawe na 2/3 ya wabunge ili waweze kufanya watakalo.Ni jambo la hatari mno na deep root state (Serengeti wameweza)watusaidie kuhakikisha kuwa hila hazitumiki kulifanikisha hilo kwa mustakabali mwema wa nchi.
Tulishaishi kama Chama Kimoja na faida na hasara tuliziona tusirudi tena huko,tuipalilie demokrasia ikue na tuongeze uhuru wa watu wetu.
Kampeni njema,amani na usalama wa watu wote uwe kipaumbele chetu.