chawa wa mama
JF-Expert Member
- Jun 8, 2020
- 292
- 1,084
Nimefuatilia kwa miaka mingi sana, kuna ukanda unahisi unatengwa, hawajatoa rais, na wana kiu sana ya kupata rais wa kutoka ukanda wao. wamesahau wamewahi toa mawaziri wakuu wawili.
Ukanda mwingine, wao wamepata bahati ya kupata mtu wa ukanda wa kwao aliyekuwa anawapendelea kwa kupeleka miradi, ajira, vyeo vya kuteuana nk.
Hakika kundi hili wanaumia sana na wanatapatapa sana, wamepigwa na mshale wa sumu jichoni,. Kambi yao imepukutika yote mithili ya mawaa.
Wamebaki na hasira tu na kutukana mitandaoni, wamevurugwa.
Kundi lingine ni wafia dini, kila akiingia rais wa dini flani hawamtaki, wanamtaka wa dini yao. Uzuri ni kuwa rais wa kutoka dini hiyo kwa miaka yote huwa hawana vinyongo, kutesa wala inda.
RAI.
Tunapokosoa kama taifa tujikite ktk kushauri na kutafuta suluhu ya matatizo, sio kuzomea ili aonekane rais kashindwa atoke aingie unayedhani unampenda wewe.
Tukosoe kwa nia njema.