Katika Maisha kuna wakati unafika unaacha vitu fulani

Mdoe Snr

Senior Member
Joined
Mar 5, 2014
Posts
115
Reaction score
30
#KUACHA

Kwenye maisha inafika hatua ni lazima #UACHE.Ni lazima uache yale Mambo yote ambayo kwa kiasi kikubwa yanakuzuia kufika kwenye #Mafanikio yako.

Mara nyingi Mambo ya kuacha ni yale ambayo yanatupa burudani na ya kupendeza.Yanaweza kuwa ni starehe zetu ambazo tumezifanya kwa miaka mingi na kugeuka kuwa sehemu ya maisha yetu. Yaweza kuwa ni tabia zetu ambazo kwazo tumepata sifa mbele za marafiki lakini hazina Utukufu mbele za Mungu.

Kitu cha kuelewa ni kwamba, Kuna maumivu makali na gharama kubwa katika kuziacha kwasababu kwa muda mrefu zimekua sehemu muhimu ya Maisha yetu. Moja Kati ya gharama hizo ni kupoteza Marafiki na kadhalika.

Kwahiyo ndg yangu Kama unadhani lipo Jambo au tabia yoyote ambayo unaifanya kwa mazoea lkn inakuzuia #kuendeleambele katika maisha yako, basi ni vema #Ukaiacha.

#PAMOJA na maumivu makali utakayo yapata katika #KUACHA jambo na tabia uliyoizoea, lakini ndio dawa hiyo . #ACHAA.
 
Ishara moja ya wapo ya kukua kwa mtoto ni pale anapoacha kunyonya.... so kuacha mambo yasiyo na faida kwa wakati fulani ni ishara ya kukua kwa mwanadamu....


NAWEKA UHUNI CHINI - CHindo Man
 
Ishara moja ya wapo ya kukua kwa mtoto ni pale anapoacha kunyonya.... so kuacha mambo yasiyo na faida kwa wakati fulani ni ishara ya kukua kwa mwanadamu....


NAWEKA UHUNI CHINI - CHindo Man
yanafaida kwa mfanyaji ndio maana anakuwa bado anayafanya
 
hata ukiyacha kwa lengo la kutafuta mafanikio,mwisho wa siku baada ya kupata hayo mafanikio-mafanikio hayo yatakupelekea kurudia yale yale uliyoyaacha.maana mwisho wa mafanikio yote ni kupata furaha na furaha ndio hayo mambo ambayo watu hufanya
 
Kuna vitu vingine mtu vigumu kuacha ingali anajua sio vema anafanya tu kwa sababu ni kawaida kwake
kwa mfano mtu mwingine bila kuongea kwa sauti ya juu(kupayuka) anaona hayuko sawa
japo umenena jambo jema tuko pamoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…