Katika marafiki ulio nao wangapi ni marafiki zako?

Kuna mkali mmoja alikuwa mkubwa kwangu ila tulikuwa tumeshibana haswa. Changu chake, chake changu. RIP Kamanda kaka mkubwa S. L
 
Kumbuka Urafiki wa kweli hauna gharama mboni ya jicho haijawahi kumficha rafiki wa kweli
 
Tukubali tukatae urafiki wa kweli unaweza kuwepo Kama dhana tu.ila kiuhalisia ni ngumu kiasi chake,hata mkeo wa ndoa au ndugu wa damu wakati wa shida anaweza kukukimbia au akajitenga na wewe.

Hali ya maisha pia inachangia kukosekana urafiki wa kweli .huo wakati wa shida rafiki hawezi kuvumilia kipindi chote kwa sababu na yeye pia Ana shida zake anazopapambana nazo.Hua naamini Kuna rafiki wa nyakati Fulani na wanaokuja kwa sababu Fulani

Jaribu kufikiria wakati wa Yesu anaenda kusulubiwa hakukuwa na mwanafunzi wake hata mmoja au rafiki zake Kina Magdalena na Martha ambao wangeweza kumsaidia kubeba msalaba kuelekea Golgotha.hawa ni watu aliokuwa kipindi kirefu na wengine walisema wapo tayari kufa kwa ajili yake .ulipofika wakati wa kusulubiwa wote walimkimbia

Aliyekuja kumsaidia msalaba ni mtu mwingine mpita njia ambaye hakuwahi kufahamiana naye kabla.lakini baada ya ufufuo Yesu aliwatokea wanafunzi wake Tena.hakujali marafiki wa karibu walimtenga wakati wa shida.

Hivyo la muhimu ni kujua kusudi la Kila rafiki kwenye maisha yetu.hii itatufanya kuondokana na lawama kwa Kila watu wetu wa karibu.
 
Ni rafiki zetu ,tunaoshare nao moment zetu nzuri na mbaya tunawaita katika shida na raha Ila mwisho wanatusaliti Hawa ni bayuda Kaka ,sijui utaiwekaje kwa kiswahili ndugu

Bayuda tuyita nabo ,tulala tuseka nabo Ila ni masnitch
Expert nimependa hiyo mistar ya mwisho hapo chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…