GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
- Thread starter
- #21
Haa! Mkuu na wewe sasa! Unajuaje kama nitakuja kama msomaji tu?Leo nitakujibu katika kila uzi ,ili ukirudi mwezi wa nne uje na madini zaidi na zaidi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haa! Mkuu na wewe sasa! Unajuaje kama nitakuja kama msomaji tu?Leo nitakujibu katika kila uzi ,ili ukirudi mwezi wa nne uje na madini zaidi na zaidi
Tunaomba sana uje Kama mwandishiHaa! Mkuu na wewe sasa! Unajuaje kama nitakuja kama msomaji tu?
Sawa, kama nitakuwa na cha kuandika!Tunaomba sana uje Kama mwandishi
Kumbuka Urafiki wa kweli hauna gharama mboni ya jicho haijawahi kumficha rafiki wa kweliKuwa na idadi kubwa ya wanaokushangilia kipindi ukiwa unaelekea kushinda hakumaanishi una marafiki wengi! Siku utakapoupoteza ushindi ndiyo utashangaa kuwa katika watu mia moja ulioamini ni marafiki zako, walio marafiki zako kweli, pengine hawafiki hata kumi!
Inawezekana ofisini kwako unaheshimika sana, lakini siku utakayoacha kazi inawezekana hata aliyekuwa "mdogo" sana kazini kwenu akakuonesha dharau hadharani!
Nilishangaa sana miaka ya nyuma, baada ya kuwa nje ya ajira kwa muda, baadhi ya watu nilioamini ni marafiki zangu hawakutaka hata tena mawasiliano nami.
Nakumbuka mmoja wa marafiki zangu tokea tukiwa sekondari, aliahaidi kuniazima kiasi fulani cha fedha. Lakini nilipomtafuta baadaye kwa ajili ya kumkumbusha hilo, simu yangu haikupokelewa. Nilikuwa nikipiga simu Asubuhi, Mchana, na hata Usiku lakini ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa, na wakati mwingine ilikuwa ikikatwa. Niliamua kutuma sms, lakini nazo hazikujibiwa, japo nilituma zaidi ya mara moja.
Nilipobaini kuwa jamaa kaamua kunikwepa, nilimtumia sms kuwa kuhusu hela niliyotaka kumkopa asisumbuke tena kwani nilishapata suluhisho, lakini hata hiyo nayo haikujibiwa.
Kwa kipindi cha kama miaka miwili hivi hatukuwa tukiwasiliana, japo hapo kabla ya kumshirikisha changamoto yangu, muda ulikuwa haupiti bila ama yeye kunitafuta au mimi kufanya hivyo. Lakini baada ya muda wa miaka miwili au mitatu hivi kupita, alinitumia sms kunisalimia, na mimi nikaijibu kwa amani tu, kwa sababu hata hivyo hatukuwa na uadui. Yeye aliamua kunikwepa kwa ajili ya kuepuka kuniazima fedha zake.
Kipindi hicho hicho, kuna watu ambao nilishawahi kuwasaidia, tena mwingine niliwahi kwenda kukopa hela ili nisaidie kutatua changamoto aliyokuwa nayo. Lakini mimi nilipokuwa nimebanwa, hakuuonesha mwitikio kama niliokuwa nao kipindi alipokuwa na shida. Jibu lake yeye lilikuwa jespesi tu, "nilikuwa nazo ila nimeshaagzia mzigo". Muda huo mimi nilikuwa natafuta hela ya mgonjwa aliyekuwa amelazwa hospitalini, lakini yeye alipokosa hela ya kumalizia malipo chuoni, nilienda kukopa ili tu kumsuport asiahirishe mwaka.
Japo nilikuwa najua kuwa watu huwa wanabadilika kipindi cha changamoto, kipindi hicho ndiyo nilishuhudia kwa ukubwa zaidi!
Marafiki wa kweli hujulikana kipindi cha shida. Pamoja na wengi kunikimbia kipindi hicho, wachache walisimama nami kipindi chote cha "mateso" yangu! Walikuwa hawafiki hata kumi!
Hao ndiyo ninaowaita "marafiki". Hawabadilishwi na mazingira!
Wewe unao marafiki wangapi?
Expert nimependa hiyo mistar ya mwisho hapo chiniNi rafiki zetu ,tunaoshare nao moment zetu nzuri na mbaya tunawaita katika shida na raha Ila mwisho wanatusaliti Hawa ni bayuda Kaka ,sijui utaiwekaje kwa kiswahili ndugu
Bayuda tuyita nabo ,tulala tuseka nabo Ila ni masnitch