Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Katika Mahojiano Maalum na Mwananchi, Aprili 7, 2024, Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu amesema moja ya sababu kubwa za Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa ni kutokumaliza au kutotumia Dawa vizuri hasa za Antibayotiki.
Prof. Nagu amesema mtindo wa kuwaandikia Wagonjwa Dawa 1x3 au 1x2 unapaswa kukemewa kwasababu mtu asipoelewa anaweza kutumia dozi vibaya, hivyo kusababisha janga la Magonjwa ya kuambukiza kutokana na usugu wa vimelea dhidi ya Dawa.
Amewakumbusha Watoa Huduma kutoa na kuwaandikia Wagonjwa maelezo sahihi ya Dozi pale inapobidi.