Katika Mahojiano Maalum na Mwananchi, Aprili 7, 2024, Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Tumaini Nagu amesema moja ya sababu kubwa za Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa ni kutokumaliza au kutotumia Dawa vizuri hasa za Antibayotiki.
Prof. Nagu amesema mtindo wa kuwaandikia Wagonjwa Dawa 1x3 au 1x2 unapaswa kukemewa kwasababu mtu asipoelewa anaweza kutumia dozi vibaya, hivyo kusababisha janga la Magonjwa ya kuambukiza kutokana na usugu wa vimelea dhidi ya Dawa.
Amewakumbusha Watoa Huduma kutoa na kuwaandikia Wagonjwa maelezo sahihi ya Dozi pale inapobidi.
Sawa sawia, ili kuepusha usugu wa vimelea kwa dawa za viuavijasumu.
Lakini pia serikali iangalie, usugu wa madawa unaweze kuongezeja kutokana na watu kutupa dawa bila kufuata utaratibu. Mfano: chupa ya dawa ya maji isiyokwisha mwananchi wa kawaida akaitupe wapi?
Dawa hizi zikizagaa ovyo zaweza kupelekea usugu wa madawa wa kwa haraka zaidi hata ya dozi. Maana wadudu waliopo katika mazingira watafundishwa usugu kwa kiwango kidogo cha dawa na hatimaye nao watafundishana na wadudu wenye kuathiri wanaadamu na mifugo. Hatari sana
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) S.L.P 1253 Dodoma / 77150 Dar Es Salaam. Barua pepe: info@tmda.go.tz Tovuti: www.tmda.go.tz Yah: PENDEKEZO LA UTARATIBU WA KUSHUGHULIKA NA DAWA ZISIZOFAA KWA MATUMIZI NCHINI Baadhi ya tafsiri: Dawa zisizofaa kwa matumizi: Ni zile bidhaa...