funaku
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 39,468
- 31,952
Nia nzuri ya CCM kutaka kuondoa kiu ya waliokuwa wanashinikiza na kuanikiza katiba mpya inaenda kuondoka rasmi.
CCM kupitia Rais Kikwete ilijaribu mchakato wa kuhuisha Katiba lakini ilishindikana kutokana na mgogoro na tamaa za wanasiasa.
Miaka mingi baadaye CCM kupitia Rais Samia ikachukua hatua ya kipekee yaani kuweka Katika Ilani yake 2025-30 Kujibu "kiu" ya wanaoitwa wanaharakati na wapinzani.
Hata hivyo wapinzani na wanaharakati wali-abuse nia njema ya Mhe. Rais Samia kama mwenyekiti wa CCM lakini pia aliyewahi kuwa mwenyekiti katika mchakato wa kuhuisha katiba miaka ya nyuma.
Hukumu ya haki ..Rais Samia ndiye aliyekuwa mtu pekee ambaye angeweza kuileta katiba mpya iwapo CCM,CDM na wanaharakati wangempa nafasi ya stahiki ya kutekeleza nia hiyo.
Ni bahati mbaya sana CDM ,wanaharakati na baadhi ya wanamtandao ndani ya CCM waliamua kubadili gia angani na kutaka kumchukulia cheo chake halali kilichopangwa na Mwenyezi Mungu.
Yaani watajwa hawa waliamua kujiondoa kwenye agenda za kuijenga nchi na wakaamua kujikita kwenye uroho wa madaraka wakiamini Rais Samia ni Mwanamke au ni dhaifu.
Toka anaanza kuingia madarakani wanaharakati,wanamtandao,wapinzani uchwara wameendelea kuishi kwenye "delusion" ya kwamba Rais Samia hakuandaliwa au hakuwa na uwezo huo wa kuongoza nchi.
Katika hotuba yake ya awali kabisa Rais Samia aliweka wazi kuwa ...YEYE NI NDIYE AMIR JESHI MKUU ...hii ilikuwa ni kuwakumbusha wasio waamini kwamba alikuwa tayari na aliridhia rasmi kusimama kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikimaanisha yupo tayari kukabiliana na vibweka ,uhuni ,majaribu ,dhihaka na matusi kutoka kona zote za ndani na nje ya Taifa ...na yupo tayari kutekeleza kwa maslahi ya watanzania.
Wapuuzi,vibaraka na wanaccm uchwara wakataka kujinufaisha na upole na upendo wake.
kwa muktadha wa sasa ni maoni yangu kuwa haiwezekani kuingia kwenye mchakato mwingine wa kuitafuta Katiba mpya kwa sababu we are so much polarised ...yaani tuna mabishano makali yasiyo na muafaka ...hivyo zoezi hili la katiba mpya halitowezekana hadi tutakapokuwa na maridhiano na utulivu .
Kwa ufupi...URais ni taasisi na hakuna mburula yoyote anaweza kupambana dhidi yake.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!