Katika mkakati wa PPP ya Kafulila serikali isijenge stendi na masoko.

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Serikali sasa iachane na ujenzi wa stendi za magari na masoko. Haya ni mambo yanayoweza kufanywa na watu binafsi na pia hakuna maana tena ya kujenga majengo makubwa ya kukufanya watu pamoja kama stendi na masoko.

Serikali sasa ijikite katika kujenga miondombinu ya reli na viwanja vya ndege ambapo kampuni binafsi ni vigumu kuwekeza. Mambo rahisi iwaachie watu binafsi.
 
Swali ni je sekta binafsi ya Bongo ina huo uwezo?
Inaweza, masoko ni biashara ya fremu tu. Kampuni tatu za mabasi wanaweza kujicha ga kutengeneza stendi yao. Hizo Ofisi zao pia binafsi ni Bora kuliko stendi nyingi za serikali.
 
Unazungumzia ofisi za kukata tiketi au huduma za stendi?
 
Serikali sasa iachane na ujenzi wa stendi za magari na masoko. Haya ni mambo yanayoweza kufanywa na watu binafsi na pia hakuna maana tena ya kujenga majengo makubwa ya kukufanya watu pamoja kama stendi na masoko.

Serikali sasa ijikite katika kujenga miondombinu ya reli na viwanja vya ndege ambapo kampuni binafsi ni vigumu kuwekeza. Mambo rahisi iwaachie watu binafsi.
Hapa tumbiri alikuwa nusu mtu alizungumza point ila sijui kama walimuelewa
 
Huduma za stendi ni zipi ?
Ni pamoja na mifumo ya usalama (mizani ya mabasi, ukaguzi wa Polisi/Sumatra), maegesho ya dharura ya malori, na miundombinu ya zimamoto. Kampuni binafsi itagharimia vipi askari na usalama wa abiria elfu tano kwa siku?
 
Hakuna mizani ya mabasi kwenye stendi yoyote ya serikali,
Ukaguzi wa polisi, SUMATRA na makororo mengine yote unaweza kufanyika kama vile malori na gari nyingine zisizo mabasi ya abiria unavyofanyika nje ya stendi kokote barabarani,
 
Kampuni binafsi itagharimia vipi askari na usalama wa abiria elfu tano kwa siku?
Usalama gani wa abiria unaohitaji askari kuwepo muda wote? Chukulia stendi ya serikali kama shule au hospital za serikali na stendi/Ofisi binafsi za mabasi kama shule na hospital binafsi. Zote usalama ni ule ule tu.
 
Hakuna mizani ya mabasi kwenye stendi yoyote ya serikali,
Ukaguzi wa polisi, SUMATRA na makororo mengine yote unaweza kufanyika kama vile malori na gari nyingine zisizo mabasi ya abiria unavyofanyika nje ya stendi kokote barabarani,
Utakuwa unaishi nchi ya kufikirika wewe, ushauri wako ukifuatwa, tutarajie ajali kila siku.
 
Usalama gani wa abiria unaohitaji askari kuwepo muda wote? Chukulia stendi ya serikali kama shule au hospital za serikali na stendi/Ofisi binafsi za mabasi kama shule na hospital binafsi. Zote usalama ni ule ule tu.
Unafananisha shule na stendi? Hii ni akili au matope?
 
Back
Top Bottom